2016-08-12 15:30:00

Papa aomboleza kifo cha Mstaafu Askofu Edwad Kavin Daly


Baba Mtakatifu Francisko kwa masikitiko alipokea taarifa ya kifo cha Mstaafu Askofu Edward Daly , wa Jimbo la Derry Ireland , aliyekuwa na umashuhuri wa kipekee katika kusitisha  mzozo wa kisiasa  Ireland Kaskazini. Na bila kuchelea alituma salaam za rambirambi kwa ndugu wa Marehemu, na  kwa Askofu Donald Mackeown wa jimbo la Derry , Mapadre, Masista na wote waliogushwa na msiba huu. 

Papa Francisko akikumbuka ukarimu na ari katika utume wa Askofu Daly, amemtaja kuwa mtumishi wa amani na haki, Kwa Utakatifu wake, Papa  anaungana  na watu wa Ireland  kumshikuru Mungu kwa  kulizawadia Kanisa lake zawadi ya maisha ya  Askofu Daly na hasa roho yake iliyokuwa imejaa  upendo na huruma ya Mungu Baba yetu.  Papa amemwombea pumziko la amani katika mikono ya Bwana. Pia anawaombea  wote wanao omboleza   kifo cha marehemu Askofu Daly, na amewapa baraka zake za kitume katika ahadi ya faraja na tumaini la Bwana Yesu Kristo

Marehemu Askofu Daly  alizikwa Alhamisi 11 Agosti 2016,  baada ya Ibada ya Misa ya wafu na maziko  iliyoongozwa na Askofu Donald Mackeown  Askofu wa sasa wa Jimbo la Derry , ibada iliyofanyika  katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Eugene.  . Mwanzoni mwa Misa Askofu Mkuu  Amaury Madina Blanco, Nunsio wa Papa nchni Ireland , alisoma ujumbe wa rambirambi  uliotumwa na Papa Francisko.

Marehemu Askofu Daly alifariki tarehe 8 Agosti , akiwa na  umri 82 , baada ya kuugua kwa muda mrefu. Katika homilia yake , Askofu  McKeown, alimkumbuka Marehemu kwamba ni mfano wa kuhani katika utumishi wa Mungu na wa watu. Aliweza kuhubiri injili ya amani katika nyakati ngumu na daima moyo wake ulikuwa na  nafasi ya kupokea na  kusaidia yoyote kihali na kiroho pia. Alikuwa ni mtu mkweli na muwazi .  

Askofu Daly alizaliwa Belleek, katika Jimbo la Clogher, Desemba 5, 1933. Alipadirishwa mwaka  1957 na kuwa Askofu wa Derry 1974-1994. Alistaafu kazi ya kuliongoza Jimbo la Derry  baada ya kushikwa na ugonjwa mbaya uliomlazimisha kustaafu. Hata hivyo , pamoja na matatizo ya afya,  aliendelea kufanya kazi kama mchungaji katika Jimbo la Derry na pia kama Mkutubu wa Jimbo. Askofu Daly anatajwa pia kuwa  alama ya "Matatizo ya Ireland ya Kaskazini, mzozo wenye umwangaji wa damu  uliopamba moto hasa  mwaka 1972, ambamo  watu  14 waliuawa mjini  Derry kwa kupigwa risasi na askari wa Uingereza.








All the contents on this site are copyrighted ©.