Mtandao wa kidini dhidi ya unyonyaji wa kigono kwa watoto na vijana na usafirishaji haramu wa watu, juhudi zilizoanzishwa miaka miwili iliyopita, wakati wa Kombe la Dunia , kampeni hiyo , imeendelezwa pia kwa nguvu katika kipindi hiki cha michezo ya Olympiki, inayoendelea Rio de Janeiro Brazil. Juhudi hizi dhidi ya usafirishaji wa watu "Um Grito pela vida" zinaendelea chini ya Kauli mbiu: ”Kucheza kwa ajili ya maisha”. Na kama ilivyokuwa mwaka 2014, lengo lake linaendelea kuwa ; ni kukabiliana na matendo yanayo nyanyasa heshima ya binadamu, yaliyoenea katika kila kona ya dunia ya uraiani na utalii.
Msimamizi wa Kampeni hii ”Talitha Kum”, Sista Alves se Oliveira, amenukuliea na gazeti la L’Osservatore Romano akieleza kwamba, huu ni mtandao wa kimataifa wa jumuiya za dini, katika lengo la kupambana na usafirishaji haramu wa watu, juhudi zinazoungwa mkono na Umoja wa Kimataifa wa Wakuu wa Mashirika ya Watawa, kama mfumo kuelimisha , kufahamisha na kuwawezesha wananchi, vyombo vya habari na vyombo vya usafiri kwamba, inawezekana kuzuia dhuluma hizi zinazofanywa na watu dhalimu na walaghai.
Sista Alves amesema, wanalenga kuitumia michezo hii ya Olympic ya Rio 2016, kama nafasi ya kuelimisha umma, maana ya kuwa uraia mwema, huduma katika maisha na kukana aina zote za mitengo na ukiukwaji wa haki za binadamu hasa kupitia usafirishaji haramu, kwa kutoa zana kwa wakazi, ili waweze kuinua zaidi ufahamu wao, hivyo kuguswa na kukemea aina zote za biashara yenye kuwa na mwelekeo wa kuvunja heshima ya maisha ya binadamu .
Na kwamba inahusu kuchukua msimamo thabiti dhidi ya majeshi ya kifo na kuthibitisha dhamira katika neema ya kutetea na kuyalinda maisha, hasa kwa wale ambao , haki zao zinakiukwa na kuwafanya waishi chini ya minyororo wa utumwa wa kisasa, kama Papa Francis alivyoliita 'pigo katika mwili wa binadamu'.
Kampeni hii inayopambana na usafirishaji haramu wa watu , inaendeshwa na vikundi 26 katika mtandao katika mikoa 22 ya Brazil. Inatoa wito kwa watu wote, kukemea na kuwafikisha wote mbele ya sheria , wote wanaobainika kuwa na nia za kujihusisha na uhalifu huu dhidi ya ubinadamu. Kampeni inafanyika kupitia vyombo vya habari na mawasiliano vya kijamii. Ni kampeni inayofanyika katika mitaa ya Rio de Janeiro na Manaus. Pia kupitia mitalaa ya elimu hasa kwa watoto na vijana, ambao ni makundi malengwa zaidi yanayotafutwa na walanguzi na wanyonyaji wa watu.
All the contents on this site are copyrighted ©. |