2016-07-27 09:40:00

Vatican: mkataba wa ushirikiano kati ya AIF na Benk Kuu ya Italia


Mamlaka ya habari za fedha ya Vatican  (AIF) na Benki Kuu ya Italia, wamehitimisha mchakato wao kwa   mkataba wa ushirikiano,  ili kuwezesha kimsingi, kubadilishana habari zinazohusiana na usimamizi wa fedha.  Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Ofisi ya habari ya Vatican, Mkataba unaruhusu wote wawili,  kupanua mawasiliano kwa ajili ya kufuatilia uhusiano uliopo,  kati ya  waamuzi wa Italia na taasisi za kitaaluma, zinazohusiana na shughuli za fedha katika JimboTakatifu na Vatican. Na kwamba kumeweka kati ya mengine, vifungu vinavyohusiana na usiri na matumizi ya habari.  Mkataba huu wa ushirikiano ni nyongeza kwa mikataba mingine ambayo tayari ilikwisha pitishwa na kuwekwa saini tayari kati ya AIF and Kitengo cha Usalama wa Fedha  (FIU) cha Italia mwaka 2013 kwa ajili ya ushirikiano,  katika kuzuia na kupambana na fedha haramu na ufadhili wa ugaidi. Mkataba huo ulisainiwa kwa upande wa  AIF, na Rais René Brülhart na Tommaso Di Ruzza Mkurugenzi; na upande wa  Benki Kuu ya Italia Gavana Ignazio Visco na Mkuu wa Idara ya Usimamizi, Carmel Barbagallo.

Juhudi hizi za usimamizi makini  na udhibiti wa  fedha katika  Jimbo Takatifu na Vatican ,  zilizounda AIF,  zilianzishwa rasmi na Papa Benedict XVI 30 Desemba 2010 na kuimarishwa na Papa Francis kwa Mkataba Novemba 15, 2013.

AIF, hadi sasa imesaini makubaliano ya ushirikiano na mamlaka za usimamizi wa fedha za nchi mbalimbali za kigeni, ikiwa ni pamoja Brazil, Ujerumani, Luxembourg, Poland na Umoja wa Mataifa ya Amerika. Mamlaka inayohusika na taarifa za fedhaya  "Egmont Group, na pia makubaliano ya ushirikiano na kitengo cha usalama wa Fedha cha  (FIU) katika  nchi mbalimbali za kigeni, ikiwa ni pamoja Albania, Argentina, Australia, Austria, Ubelgiji, Brazil, Canada, Cyprus, Cuba, Ufaransa, Ujerumani, Italia, Lichtenstein, Luxembourg, Malta, Monako, Norway, Uholanzi, Paraguay, Peru, Poland, Uingereza, Romania, San Marino, Slovenia, Hispania, United mataifa ya Amerika, Afrika Kusini, Uswisi, Hungary.








All the contents on this site are copyrighted ©.