2016-07-27 09:54:00

Mkusanyiko wa Vijana Krakow Poland ishara ya amani na Umoja


Wakati dunia ya watu wema imejazwa na majonzi kwa vitendo vya kigaidi sehemu mbali mbali za dunia, mjini Krakow Poland, vijana wanaendelea kumiminika maelfu kwa maelfu  kwa ajili ya maadhimisho Siku ya Vijana ya XXXI ya Vijana ambayo inafanyika sambamba na maadhisho yao ya Jubilee ya mwaka wa Huruma ya Mungu, changamoto kwa vijana kuwa ni mashuhuda, vyombo na mitume wa huruma ya Mungu kwa waja wake.

Kardinali Stanslaw Dziwisz, Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Krakow Poland , amelitaja adhimisho hili la Siku ya Vijana ya Dunia kuwa ni ishara ya amani na umoja kwa dunia. Kwao ni furaha kuu, kwa Papa kukubali mwaliko wa vijana wa kushiriki pamoja nao katika adhimisho hili. Na kwamba , wanakumbuka miaka 25 iliyopita mjini  Czestochowa, kwa mara ya kwanza, kulifanyika tukio katika ngazi ya kikanda ,lililo hudhuriwa na vijana zaidi ya 200,000 kutoka nchi za Ulaya Mashariki ikiwemo Urusi, Ukraine. Huu ni wakati wa kujifunza wote kwa pamoja, jinsi inavyowezekana kuwa pamoja na  ushiriki sawa wa  imani, furaha na saka na maonbi kwa matumaini ya siku za baadaye. Ni tukio la kuvutia na kutia nguvu mpya katika misingi ya maisha ya  imani na furaha ya kuwa Wakristo.

Katika mahojiano,  Kardinali Diswisz ameonyesha matumaini yake kwamba, hii ni ishara kubwa kwa vijana kujenga umoja na amani na maisha ya mshikamano na huruma. Mkusanyiko huu ni mahali pa kuanzia kutoa kilio cha amani na ujenzi wa uhusiano mzuri kati ya watu na mataifa. Kanisa, katika nchi mbalimbali,  lazima kuwa na mwamko wa kusikiliza kilio cha vijana wema wanataka nini. Ni lazima waamini kujenga Kanisa halisi la maskini na majonzi kama ulivyo ukweli wa Kanisa la karne ya kwanza.








All the contents on this site are copyrighted ©.