2016-07-25 09:22:00

Papa: Kutanguliza neno Baba katika sala ni kumtamguliza Mungu katika yote


Baba Mtakatifu Francisko Jumapili katika hotuba yake kabla ya sala ya Malaika wa Bwana, alilenga katika mafundisho ya Yesu juu ya maombi, kama ilivyotajwa katika somo la Injili ya siku. Mitume walimwomba Yesu awafundishe jinsi ya kuomba.  Na Yesu alijibu, "Mnaposali, semeni  'Baba  yetu...Papa alifafanunua kwamba, kwa kuanza na neno hili "Baba," mna “siri" ya sala ya Yesu ambayo inakuwa ni ufunguo  muhimu  anaowapa waamini wake yeye mwenyewe,  ili pia waweze kuingia katika uhusiano huo wa mazungumzo ya siri na Baba wa Mbunguni .Wakati wote wa maombi ni muhimu kukumbuka kwamba ni wakati wa muhimu wa mazungumzo kati yangu na Mungu. 

Aliendelea kuelezea juu ya sala ya Bwana  kwa Mungu, akitaja kwanza aya mbili, "Jina lako litukuzwe," na "Ufalme wako uje”akisema  kwamba, zinahusiana na jina "Baba. Katika sala hii ya Bwana ambayo ni  sala ya Mkristo, inafundisha kwanza kabisa  kutoa kipaumbele  kwa Mungu, katika utendaji wote wa  maisha yetu.

Katika Injili ya Luka, Sala ya Bwana inaendelea kuomba mahitaji mengine msingi katika maisha ya binadamu ambayo ni : chakula, msamaha, na msaada wakati wa majaribu. “Tunaomba katika sala ya Bwana , utupe mkate wetu wa kila siku, kwa kuwa chakula ni muhimu katika maisha yetu.  Na pia tunaomba msamaha kwa  dhambi zetu  wenyewe, ili tuweze kupata nguvu ya kusamehe  wengine pia  wanaotukosea na hivyo kutenda kwa uthabiti katika  maridhiano ya kidugu na tunaomba msaada wa Mungu uweze kutuongoza wakati tunapojaribiwa, kwa sababu tunajua sisi ni dhaifu mbele ya mitego ya uovu na ufisadi.

Papa Francisko aliendelea kutoa ufafanuzi kwa mifano miwili iliyofuatia mafundisho ya Bwana  juu ya akisema mifano hiyo inalenga kutufundisha sisi kuwa na imani kamilifu kwa Mungu ambaye ni Baba. Na kwamba Mungu hahitaji maombi yetu katika kujua nini tunahitaji, au kumshawishi atupatie kile tunachokihitaji.  Badala yake, Papa Francisko amesema, tunaomba, ili imani  na uvumilivu wetu uweze kuimarishwa, ili tuweze kupambana pamoja na Mungu kwa mambo muhimu zaidi tunayohitaji.

Papa alieleza na kuongeza kwamba, kwa bahati mbaya , daima hatukumbuki kuomba kujaliwa kingine kilicho cha muhimu zaidi, ambaye ni Roho Mtakatifu.  Kuomba zawadi ya Roho Mtakatifu, ili atusaidie kuishi vizuri, kuishi kwa hekima na upendo, kutenda kwa kudra ya Mungu. Papa alieleza na kutoa wito kwa watu wote, katika wiki hii, kila mmoja wetu amwombe Baba, zawadi ya Roho Makatifu.

Baba Mtakatifu alikamilisha kwa kugeukia matukio ya kusikitisha yanayoendelea kuisononesha mioyo ya watu, utendaji wa kigaidi na ghasia za mauaji, akiwakumbuka wahanga wa shambulio lililofanyika mnjini Munich Ujerumaninahuko Kabul Afghanistan, ambamo makumi ya watu wsiokuw ana hatia wamepoteza maisha na wengine wengi kubali majeruhi. Papa alisema kiroho yu pamoja nao wote na akatoa mwaliko kwa wote kuungana nae katika sala za kumwomba Bwana awavuvio wote roho wa mapendo na udugu.  Na akakumbusha kwamba pale panapokuwa na matatizo makubwa, usalama na amani hufunikwa na uvuli wa giza, unaohitaji kuondolewa kwa njia ya maombi.   

Baada ya sala ya Malaika wa Bwana, Papa pia aliikubuka Siku ya Vijana ya Dunia, itakayo adhimishwa huko Krakow Poland, tangu tarehe 25-31Julai 2016,  ambako pia yeyé mwenyewe anatazamia kwenda huko tangu siku ya Jumatano ya wiki hii, kuungana na vijana toka pande mbalimbali za dunia.  Kusherehekea pamoja nao Jubilee yao ya Mwaka wa Huruma, kwa maombezi ya Mtakatifu Yohane  Paul II. Papa ameomba sala la waamini ziongozane nao wote katika tukio. Mpaka sasa zimeanza  kazi za kuwapokea mahujaji vijana, wakiwa wameongozana na maaskofu , mapadre, watawa, walei. Papa alitoa pia  salamu zake za  kipekee kwa vijana wenzao wengi ambao, hawawezi kwenda Poland, lakini amewaomba wafutane nao kupitia vyombo vya habari. Kwa njia hiyo wote wataungana  pamoja katika umoja wa maombi!








All the contents on this site are copyrighted ©.