2016-07-09 08:13:00

Papa aridhia kufanyika michakato ya watumishi wa Mungu kadhaa


(Vatican )Tarehe 8 Julai 2016, Baba Mtakatifu Francisko, alikutana na kuzungumza faraghani  na Kardinali Angelo Amato, S.D.B., Msimamizi wa Usharika kwa ajili ya Michakato ya kutaja wenye heri na Watakatifu. Katika mazungumzo yao Papa aliidhiniisha kufanyika kwa michakato kadhaa juu ya : 

-Miujiza inayohusu maombezi ya Mtumishi wa Mungu Luigi Antonio Rosa Ormières, Padre na mwanzilishi wa Usharika wa Masista wa Mtakatifu  Malaika Mlinzi , aliyezaliwa Julai 4, 1809 na alifariki tarehe 16 Januari 1890;

-Kuuawa kama Mashahidi wa dini  Antonio Arribas Hortigüela na wenzake sita , Wamisionari wa Moyo Mtakatifu wa Yesu ,waliouawa kwa chuki za kidini  Septemba 29, 1936;

-Kuuawa  kama shahidi wa  imani Giuseppe Mayr-Nusser,Mlei  aliyeuawa kwa  chuki za kidini  Februari 24, 1945;

-Fadhila za kishujaa za  Alfonso Gallegos, Shirika la Mtaktifu Augusitne Recolleti , Askofu wa Jina wa SASABE, aliyezaliwa  Februari 20, 1931 na alikufa Oktoba 6, 1991;

 Fadhila za kishujaa za Mtumishi wa Mungu Raffaele Sánchez García, Padre wa jimbo; aliyezaliwa 14 Juni 1911 na kufariki tarehe 8 Agosti, 1973;

 Fadhila za kishujaa wa Mtumishi wa Mungu Andrea Filomeno García Acosta, Mlei wa ndugu wadogo ; ayezaliwa 10 Januari 1800 na kufariki Januari 14, 1853;

- Fadhila za kishujaa za  Joseph Marchetti, Padre kuhani wa Usharika wa Wamisionari wa Mt. Charles; aliyezaliwa Oktoba 3, 1869 na kufariki Desemba 14, 1896;

- Fadhila za kishujaa za Giacomo Viale, Padre wa Shirika la Ndugu Wadogo mchungaji wa Bordighera; aliyezaliwa Februari 28, 1830 na kufariki  Aprili 16, 1912;

- Fadhila za kishujaa za  Maria Pia wa Msalaba ( Maddalena Notari), mwanzilishi wa Usharika wa Masista wa Msulubiwa Waabuduo Ekaristi; aliyezaliwa Desemba 2, 1847 na kufariki tarehe 1 Julai 1919.








All the contents on this site are copyrighted ©.