2016-07-08 09:03:00

Kesi ya Vatileaks II Maofisa wawili hatiani na wanahabari wawili huru


(Vatican Radio) Alhamisi Jopo la Mahakama ya Vatican lililokuwa likisikiliza keshi ya kuvujisha nyaraka za siri za Vatican,  iliyojulikana kwa jina Vatileaks 2, liliwaona kuwa na hatia watumishi wa Vatican wawili waliohusika katika kesi hiyo Padre Lucio Angel Vallejo Balda na mlei Francesca Immaculata Chaouqui.Na  watuhumiwa wengine wawili ambao ni  waandishi wawili waliohusika katika kesi hii, waliachiwa huru.

Padre Angel Lucio Vallejo  Balda  Mhispania,aliyekuwa Katibu wa Tume inayohusika na tafiti na ukusanyaji hbaari za Vatican na jimbo Takatifu , kwa mujibu wa mahakimu alitoa  nayaraka za siri kwa wanahabari wawili. Kwa kosa hilo  amehukumiwa kifungo cha ndani cha  miezi 18 jela akiwatakiw akubaki ndani ya Vatican. Na mwanamama Francesca Chaouqui ambaye ana mtoto mchanga wa wiki tatu, pia amepatikana na hatia na kusomewa adhabu ya kusimamishwa kazi kwa muda wa miezi kumi. 

Walio achiwa huru ni wanahabari wawili Waitaliani,  Gianluigi Nuzzi na Emiliano Fittipaldi, ambao mwaka jana waliandika vitabu viwili vyenye kuwa na nyaraka za siri za Vatican, kuvichapisha na kuviuza. Mahakama ya Vatican imewaachia huru kwa misingi ya kisheria kwamba, Vatican  haina mamlaka juu yao.

Na mshtakiwa mwingine wa tano, Nicola Maio, aliyekuwa katibu msaidizi wa Vallejo, mwishoni mwa kesi, alionekana hana hatia , katika kesi hii iliyosikilizwa kwa mara 21 katika kipindi cha miezi minane . 

 Padre Federico Lombardi, akitoa muhtasari kwa wanababari baada ya hukumu kutolewa alisema,   hukumu imetolewa kwa mujibu wa sheria ya mwaka 2013, inayohusika na uvujishaji wa nyaraka za Vatican.  Na kwamba., Mahakama imebidi kuendesha kesi hii kwa mujibu wa sheria, ili  kuonyesha dhamira ya Vatican katika  kupambana uvujishaji wa nyaraka na migogoro ya ndani ya Vatican , ambayo kwa muda  imekuwa ikijitokeza mara kwa mara  na hivyo kujenga mduara na utata  hasi  katika mazingira ya mwingiliano wa mawasiliano ya ndani  na  njia za mawasiliano ya kijamii za nje , na hivyo kuwa na  matokeo mabaya katika maoni ya umma, ambayo ina haki ya kupata habari kwa utulivu habari sahihi.  Padre Fedrico Lombardi amesema , huu ni  "ugonjwa", kama Papa Francisko alivyosema, unapaswa kupiganwa na dhamiri ya mtu mwenyewe, katika kuheshimu mazingira ya kazi yake.

Na Mtetezi wa Vatican katika kesi hii , Profesa Roberto Zannotti,naye  amesema, kesi hii, haikuwa na maana ya kupinga dhidi ya uhuru wa vyombo vya mawasiliano, lakini ni kulinda matumizi ya nyaraka za siri kama inavyodhamiriwa. 








All the contents on this site are copyrighted ©.