2016-07-07 11:27:00

Kongamano la Ekaristi Takatifu Kitaifa nchini Italia!


Baba Mtakatifu Francisko, amemwandikia barua Kardinali Angelo Bagnasco, aliyemteua kuwa mjumbe wake maalum katika Kongamano la Kiekaristi la XXVI la Kitaifa Italia, ambalo litafanyika tarehe 5-18 Septemba mwaka huu.  Kardinali Bagnasco Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Genoa, ambaye pia ni Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Italia. Baba Mtakatifu Francisko katika barua hii  ameonyesha kufurahia tarehe ya Kongamano iliyopangwa, ambalo litaadhimishwa Jimbo kuu la Genoa, Kaskazini mwa Italia, kwamba litawezesha mahudhurio mazuri ya waamini wengi,  wakiwemo Makardinali, Mapadre , watawa na Walei, kusherehekea chanzo cha maisha na utume wa Kanisa na amana ya utukufu ujao.  

Pia Papa ameonyesha imani yake kwa  Kardinali Bagnasco,  aliyemteua kama mjumbe wake maalum katika Kongamano hili la Ekaristi Takatifu Kitaifa, akimhakikishia kwamba yuko pamoja nae na pia kwamba, kwa sifa, busara, vipaji na uzoefu wake wa kichungaji, kwa msaada wa Roho Mtakatifu, ataweza kutekeleza kazi alizomdhaminisha. Barua ya Papa inaendelea kutoa himizo kwa waamini wote, washiriki na kutoa  heshima zao kwa Sakramenti Kuu, Sakramenti ya Ekaristi Takatifu: kifungo cha upendo, Karamu ya Pasaka, yenye kulisha udugu na umoja na kila mmoja katika ushirikiano wa mchakato wa kujenga Kanisa moja na kwa ajili mema ya dunia.

Na hivyo, Baba Mtakatifu anatoa  wito kwa kila mmoja kwa kadri awezavyo  na hasa katika hali ngumu za maisha,   kila siku aweze kupokea  Sakramenti hii ya  upendo mkuu wa Kristo na  huruma yake, inayohifadhiwa katika makanisa, ambayo Papa anasema  mara nyingi haitiliwi maanani wakati wa  kumzungumzia Mwana, na katika kumsikiliza kwa ukimya na katika kumtegemea  Yeye.  Hivyo Papa anatoa mwaliko kwa kanisa zina kuimba wimbo wa Sakramenti Kuu " Tantum Ergo Sacramentum veneremur cernui et antiquum documentum novo Cedat ritui” " Sakramenti kubwa hiyo twaheshimu kifudi... 

Barua ya Papa imemalizia kwa kuomba maombezi ya Mama Maria Mtakatifu sana Mama wa Mungu  , aliwezeshe Kongamano hili la Kiekaristi la Kitaifa Italia, kupata ushindi na kuzaa matunda tele ya kiroho. Na mwisho kabisa Papa  ametoa baraka zake za kutume kwa Kardinali Bagnasco na kwa washiriki wote wa Kongamano , akiomba pia sala zao kwa ajili ya utume wake katika Kiti cha Petro.

Kongamano la Kiekaristi la Kitaifa la Genoa Itala,  linafanyika chini ya kaulimbiu : Ekaristi chemchemi ya Utume : Kwa Huruma yako, umekutana na wote” Na maadhimisho yatafanyika kwa kuongozwa na Mada Kuu nne ikiwa ni : Wingi katika umoja wa imani;Sala ya IV ya Ekaristi. Kujifunua kwa Fumbo la Ekaristi yenyewe, Ekaristi na Mabadiliko ya Utume katika Kanisa. Ekaristi : zawadi ya Mungu katika kukutana na binadamu wa leo .  

 

 








All the contents on this site are copyrighted ©.