2016-07-06 14:36:00

Papa ahimiza kuwaombea wenye mioyo migumu na wasiokuwa na huruma!


Katika ukumbi wa Paulo VI wa mjini Vatican, majira ya asubuhi, Baba Mtakatifu Francisko, alikutana na kikundi cha mahujaji maskini kutoka Jimbo la Lyone Ufaransa,  wakiwa wameongozana na Kardinali Philippe Barbarin. Hija hii iliyoandaliwa na  Chama cha kukuza Urafiki kati ya Watu, kilichoanzishwa na Padre Joseph Wresinski. Hija hii imetajwa kuwa sehemu ya  kuadhimisha miaka mia ya Padre huyo, aliyeyatolea maisha yake bila kujibakiza katika kuhudumia maskini.

Hotuba ya Papa kwa mahujaji hawa , imetoa ujumbe wa kubebana bega kwa bega katika hali zote , kama ilivyo historia ya chama chao, ambayo asili yake ni wito wa Kristo mwenyewe, kuhudumiana mmoja kwa mwingine. Papa alionyesha pia furaha ya kukutana na mahujaji hawa akisema,  wote anawapokea kwa mikono miwili, na kuwataka kila mmoja wao ajisikie nyumbani, kama ndugu, na kwamba uwepo wao ni muhimu kwake pia . Na alitaja la muhimu zaidi walilokuja nalo ni Yesu mwenyewe anayewaunganisha  wote kwake. Na kama kuna kitu wanachoweza kukichota toka kwa Yesu ni huo uwezo wa upendo wake wenye kuwaunganisha wote.

Baba Mtakatifu aliendelea kuutaja uwepo wao kuwa ni ushuhuda hai  unaoonyesha uzuri wa kuishi katika mshikamano wa udugu wa kiinjili katika safari  ya pamoja ya hija ya maisha. Katika safari hii, Papa alionyesha imani yake kwamba bila sahka wameweza fika wakiwa wameandamana pamoja, wakisaidia mmoja kwa mwingine kwa  ukarimu si katika upatikanaji wa vitu na mahitaji muhimu tu lakini pia mahitaji ya kiroho, wakishirikishana Yesu mwenyewe, kwa kuwa Yesu anapenda kuishi pamoja nao katika  hali yao ,  kwa upendo wake mkuu , anaoutoa kwa kila binadamu na hakuna aliyesahaulika, au kupuuzwa.

Papa aliasa, kumbe pale panapotokea kupita katika majaribu haya ya kusahaulika au kupuuzwa, ni muhimu kutosahau kwamba, hata Yesu mwenyewe alipita katika njia hii ya kupuuzwa kama wao. Papa ameutaja kuwa huo ni ushuhuda wa thamani sana,  machoni pa Yesu,ambaye daima huwaweka moyoni mwake, ambalo ni Kanisa, kama alivyosema Padre Joseph Wresinski, kwa sababu Yesu, katika maisha yake, siku zote alitoa kipaumbele kwa watu  maskini kama wao , watu walioishi hali hiyo. Na kwamba Kanisa , lililosheni upendo, haliwezi kukaa kimya, daima huhamasika kutafuta njia ya kuwafika  wale wote ambao wanaishi katika hali za kukataliwa, kutengwa au kupuuzwa na wote.

Papa alieleza na kuwahakikishia wote kwamba, katika moyo wa Kanisa, wanaruhusiwa kukutana na Yesu, kwa sababu Kanisa halimzunguzii Yesu kwa maneno tu lakini pia ni utendaji wa maisha yake ya kila siku. Na hivyo matendo ya kawaida yenye kushuhudia upendo wa Yesu,  inakuwa ni ishara muhimu katika kumfika kila mtu, na husaidia kujenga amani na kutukumbusha kwamba sisi ni ndugu, na kwamba Mungu ni Baba wa wote.

 Baba Mtakatifu alieleza akiyaongoza mawazo  katika nyakati za kale pale wazazi wa Yesu walipokimbilia Misri, akihoji, watu walifikiri nini pale walipomwona Maria  Yosef una Yesu kama wakimbizi katika mitaa ya Misri. Bila shaka walionekana kuwa  watu maskini, maisha yao yakiwa yamejaa hofu za na mateso, lakini kumbe hapo palikuwa na Mungu.

Aidha Papa aliwageukia viongozi waliokuwa wameandamana na kundi hili , akawashukuru na kuwataka wote kuishi kwa uaminifu  uvuvio wa Padre Joseph Wresinski, aliyeyatolea maisha yake katika kukutana na kuishi na watu maskini. Aliwataka wajitahidi licha ya matatizo na changamoto zinazowakabili , waendelee kwa ujasiri kutembea katika njia hii  bila kukata tamaa. Na kwamba, Mwaka wa Huruma, iwe ni  fursa mpya ya kuishi mwelekeo wa mshikamano, udugu na kugawana  kinachopatikana na wahitaji wote.Papa amesema masiha ya kushirikishana na kugawana na maskini huleta mabadiliko na uongofu wa moyo. . 

Na aliomba Mungu anayewalinda dhidi ya ukosefu wa haki aweze kuwa faraja katika hali zote zinazosababisha mateso , wapate ujasiri wa kuvumilia matatizo yao, wakiyageuza kuwa furaha ya matumaini, ili kwamba moto wa imani unaowaka ndani yao unaendelea kuwepo bila cha kuuzimisha. pia aliwaomba wasali kwa ajili matajiri  wanaokula na kusaza bila kufikiri mbele ya milango yao kuna akina Lazaro wanaosubiri kula makombo yanayododoka toka mezani kwao. Na pia Papa amewahimiza wasali kwa ajili ya viongozi wa kanisa Maaskofu na Mapadre wao na pia kuwaombea watu wenye roho ngumu wasiokuwa na huruma, wenye kupita bila kujali mtu aliye katika hali taabani aliyelala kando ya barabara mwenye kuhitaji msaada. Na pia kwa watu wote wenye hali kama hiyo. wote ni kuwaombea ili mateso yao, yaweze kuwa faraja ya moyo , wawe na hamu ya kuomba uongofu kutoka Yesu. Baba Mtakatifu amesema , wakifanya hivyo itakuwa ni furaha kubwa kwa kanisa , na kwa mioyo yao na pia kwa taifa pendwa na Ufaransa . 

Papa alikamilisha hotuba yke kwa kuweka wote chini ya ulinzi wa Mama wa Yesu  na Mtakatifu Yosefu , na kuwapa baraka zake za kitume. Aidha mapema Jumatano hii katika Ukumbi wa Paulo VI, wakiwa pamoja na mahujaji kutoka Lyone, Papa alikutana na wazazi wa Beau Solomon, kijana Mmarekani aliyekutwa amefariki hivi karibuni katika eneo la Mto Tevere, hapa Roma. Papa alionyesha kuwa pamoja nao katika majonzi yao na pia ukaribu wake kupitia matoleo ya sala zake kwa Mungu kwa ajili kijana huyo aliyekutwa amekufa katika mazingira ya yasioeleweka. 








All the contents on this site are copyrighted ©.