2016-07-04 09:47:00

Papa Francisko awakumbuka wahanga wa mashambulizi ya kigaidi dhaka/Baghdad


Jumapili nyakati za adhuhuri baada ya sala ya Malaika wa Bwana Baba Mtakatifu Francisko, aliwakumbuka wahanga wote wa mashambulio ya kigaidi yaliyofanyika  Bangladesh na Iraki,  akiwaweka wote chini ya maombezi ya Mama Bikira Maria, Mama wa faraja na mwombezi wetu.  Papa alieleza  ukaribu wake  kwa familia za wale waliouawa na waliobaki majeruhi katika mahambulio hayo mabaya ya Jumamosi, moja katika mji Mkuu Dhaka Bangladesh na jinigine Baghdad Iraki. Aliwasihi wote kwa pamoja wasali sala ya salaam Maria kwa ajili yao, na kwa ajili ya waliofariki ,  kumwomba Bwana abadili mioyo migumu inayopenda vurugu, mioyo iliyopofusha na chuki..

Baada ya hapo, alisalimia makundi mbalimbali ya mahujaji waliofika kwa wingi kutoka sehemu mbalimbali za Italia na dunia kote akilitaja kundi kubwa lililoongozwa na Askofu wa Bergamo - Atalanta akisema kwa hakika wingi wao ni ishara wazi wa kukombozi! Na kikundi kikubwa kutoka Bragança-Miranda Ureno; pia kundi la Masista Wamisionari wa Moyo Mtakatifu toka Korea na kundi la vijana ambao wako katika  maandalizi ya kupokea kipaimara, aidha kundi laMahujaji kutoka  Venezuela. Pia  aliwasalimia raia wenzake kutoka Rioja, Chilecito Argentina waliokuwa wakipeperusha bendera yao kwa nguvu.

Pia alitoa salamu zake maalum kwa makundi yaliyokuwa yakifanya hija maalum kwa ajili ya mwaka wa Huruma , wakiwemo waamini kutoka Ascoli Piceno, ambao walikuwa wametembea mwendo mrefu kwa miguu kupitia barabara kuu ya Salaria; pia wajumbe kutoka Shirikisho la Italia la Utalii la  Equestre waliofika kwa kupanda farasi, na baadhi ya makundi kutoka Krakow; Wapanda baiskeli na pikipiki kutoka Cardito Naples.

Na mwisho kabisa alitoa salaam kwa chama cha Matumaini cha Briciole cha Carla Zichetti, Mlei mwanafamilia wa shirika la Wakamiliana , na kutoka shule ya  Chekechea ya Verdellino, na vijnaa kutoka Albino, Desenzano, na Sassari.

Pia akakumbusha kwamba , Jumatano ya wiki hii katika Mwaka huu Mtakatifu wa Huruma , tunafanya kumbukumbu ya maisha ya Mtakatifu Maria Goretti, shahidi msichana mdogo ambaye kabla ya kifo chake, alimsamehe  muuaji wake. Papa alitaja ujasiri wa Binti hiyo kwamba anasitahili kupongezwa kwa kupingiwa makofi na wote waliokuwa wamekusanyika katika uwanja huo.  Na kwao wote aliwatakia  Jumapili njema.

 








All the contents on this site are copyrighted ©.