2016-07-01 15:42:00

Tanzia: Askofu mstaafu Robert Marie Gay, WF. amefariki dunia


Askofu mstaafu Robert  Marie Gay wa Jimbo Katoliki Kabale Uganda, tarehe 29 Juni 2016 amefariki dunia huo Ottawa, Canada, alikokuwa anaishi tangu mwaka 2010. Marehemu Askofu Gay alizaliwa huko Ontario Canada tarehe 22 Januari 1927. Baada ya masomo na majiundo yake ya Kitawa na Kikasisi, akapewa Daraja Takatifu la Upadre hapo tarehe 30 Januari 1954. Tarehe 11 Januari 1996 akateuliwa kuwa Askofu wa Jimbo Katoliki Kabale, Uganda na kuwekwa wakfu kama Askofu hapo tarehe 9 Machi 1996. Tarehe 19 Februari 2003 akang’atuka kutoka madarakani. Mazishi yake yatafanyika Jumamosi, tarehe 9 Julai 2016 huko Jimbo kuu la Sherbrooke, nchini Canada.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S.

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican.

 

 








All the contents on this site are copyrighted ©.