2016-06-29 11:32:00

Mh. Padre Roberto Bergamaschi ateuliwa kuwa Vika wa Kitume Awasa!


Baba Mtakatifu Francisko amemteua Mheshimiwa Padre Roberto Bergamaschi, SDB, kuwa Vika wa Kitume wa Jimbo la Awasa, nchini Ethiopia. Askofu mteule alizaliwa tarehe 17 Desemba 1954. Baada ya masomo na majiundo yake ya kitawa na kikasisi, tarehe 13 Septemba 1981 akaweka nadhiri zake za daima na kupadrishwa hapo tarehe 2 Oktoba 1982 Jimboni Brescia na Askofu Armido Gasparini, M.C.C.J, Vika wa kwanza wa kitume Jimboni Awasa.

Mara baada ya kupadrishwa katika maisha na utume wake amewahi kupelekwa huko Ethiopia kuanzia mwaka 1982 hadi mwaka 1993 huko Dilla. Mwaka 1993- 2000 alikuwa Paroko wa Zway, Vikarieti ya Kitume ya Meki. Mwaka 1998- 2010 alikuwa ni Mkuu wa Shirika la Wasalesiani wa Don Bosco nchini Ethiopia na Eritrea. Aliwahi pia kuwa mkurugenzi wa Adwa kuanzia mwaka 2000 – 2004: Mkurugenzi wa shughuli za kitume za Wasalesiani huko Gotera Addis Ababa kuanzia mwaka 2004 hadi mwaka 2007 na Mkurugenzi wa Mekanissa, Addis Ababa kuanzia mwaka 2007 – 2009 na mwishoni, Paroko wa Parokia ya Bikira Maria Msaada wa wakristo huko Dilla na Vika wa kitume Awasa. Ni mjumbe wa Baraza la Kitume na Baraza la Wakleri.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S.

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican. 








All the contents on this site are copyrighted ©.