2016-06-20 06:38:00

Watakatifu watarajiwa!


Baba Mtakatifu Francisko, Jumatatu asubuhi, tarehe 20 Juni 2016 anatarajiwa kuongoza mkutano wa kawaida wa Makardinali wakati wa sala ya hadhuhuri, ili kupiga kura kwa ajili ya wenyeheri wanaotarajiwa kutangazwa na Mama Kanisa kuwa ni watakatifu. Wenyeheri hawa ni:

Salome Leclercq, Shahidi, Mtawa wa Shirika la Shule za Kikristo; Manuel Gonzàles Garcìa, Askofu wa Jimbo Katoliki la Palencia na Muasisi wa Umoja wa Upatanisho wa Kiekaristi na Shirika la Wamissionari wa Ekaristi wa Nazareth. Padre Lodovico Pavon, Muasisi wa Shirika la Mabinti wa Bikira Maria Mkingiwa Dhambi ya Asili. Padre Alfonso Maria Fusco, mwanzilishi wa Shirika la Watawa wa Mtakatifu Yohane Mbatizaji na mwishoni ni Elizabeth wa Utatu Mtakatifu, Mtawa wa Shirika la Wakarmeli.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S.

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican.








All the contents on this site are copyrighted ©.