2016-06-20 14:47:00

Kristo anaifahamu roho ya ubinadamu na ana uwezo wa kuiponya


(Vatican)Jumapili akihutubia wakati wa sala ya Malaika wa Bwana , Baba Mtakatifu Francisco alionyesha kujali kwamba, wafuasi wote wa Kristo wanatakiwa kutoa majibu katika changamoto za  kimaisha, na Kristo ndiye pekee jibu sahihi.

Baba Mtakatifu aliuambia mkusanyiko wa mahujaji ya wageni waliofika kumsikiliza katika Uwanja wa Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro , majira ya adhuhuri. Papa kabla ya sala ya Malaika wa Bwana alitafakari Injili ya siku ambamo Yesu aliwauliza mitume wake ; Ninyi mwafikiri mimi ni nani? 

Baba Mtakatitu aliltafakari jibu la Mtume Petro  "Wewe ni Kristo wa Mungu" akiona kwamba , kwa  jibu hilo Yesu anatambua kwamba wale kumi na wawili, na hasa Petro  wamepokea kutoka kwa Baba,  ile zawadi ya imani, na kwa sababu hiyo,  Yesu alianza kuzungumza nao kwa uwazi yale yatakayomtokea Jerusalem.

Na ndivyo ilivyo hata kwetu leo hii, Yesu anarudia upya  kuwauliza wafuasi wake, kila mmoja katika nafsi yake 'Yesu ni nani kwa watu wa nyakati zetu? Na Yesu ni nani kwa kila mmoja wetu .  Kumbe kila mmoja wetu anatakiwa kutoa jibu lake kama Petro alivyotoa jibu lake, kwa furaha na utambuzi kwamba, Yesu ni Mwana wa Mungu, Neno wa milele kutoka kwa Baba, aliyetumwa kwa ajili ya kuwakomboa binadamu, kwa kuwamwangia watu  wingi wa huruma ya Mungu. 

Papa alieleza na kusisitiza kwamba , leo hii dunia yetu inamhitaji zaidi Kristo. Inahitaji wokovu wake, upendo wake na huruma yake.  Watu wanaona utupu na wanajisikia hawana amani, wote wakihitaji kutoa majibu katika maswali mengi ya maisha na uwepo wao. Na ni Katika Kristo tu, peke ndani yake inawezekana kupata amani ya kweli na utimilifu wa kila nia za binadamu. Yesu anaujua moyo wa mtu na hakuna mtu mwingine. Hiyo ndiyo maana yeye huuponya na  kuutia uhai mpya na kuufariji.  

Papa aliendelea kutafakari sentensi ya Yesu ya kila mmoja kuubeba msalaba wake  na kumfuata akisema kuwa, hata leo Yesu anatoa mwaliko huo kwa wafuasi wake, kila mmoja auchukue msalaba wake na kumfuata.  Hii haina maana ya kuubeba kubeba ishara ya msalaba kama  pambo au itikadi,  lakini msalaba huu ina maana ya kuwajibika. Msalaba ni wajibu wa kujitolea kama  sadaka mwenyewe kwa ajili ya wengine kwa upendo, ni kuwa tayari kuishi na wengine kwa  mshikamano na hsa awale wanaopungukiwa na mahitaji yao ya lazima, watu maskini, na kuongoza  mwenyewe kwa haki na amani .

Aidha Papa alirejea aya inayosema “anayeyapoteza maisha yake kwa ajili yangu, atayaokoa” akifaafanua kwamba, ni kujiweka kikamilifu katika uaminifu wake  Yesu , ndugu yetu, rafiki na mkombozi wetu. Na kwamba kupitia Roho Mtakatifu, tunapata nguvu kusonga mbele katika njia ya imani na ushuhuda. Mwisho Papa alimwomba Mama yetu  Bikira Maria, Mama wa Yesu,  daima yu karibu na wafuasi wa mwanae wanaomruhusu kushikwa mkono nae na kuwaongoza, hasa wakati wakipita katika kipindi kigumu cha giza na ugumu wa maisha.

 

Baada ya hotuba na sala ya Malaika wa Bwana, Papa alikumbuka tukio la siku ya Jumamosi la huko Foggia,Italia, ambako kulifanyika Ibada ya kumtaja kuwa Mwenye Heri , Sista  Maria Celeste Crostarosa, mwanzilishi wa Shirika la Mtakatifu Sana Mkombozi, akisema kwa mfano wa maisha ya Mwenye Heri mpya,  na  kwa maombezi yake, iwe msaada katika kuyaweka maisha yetu yote kwa  Yesu Kristo, Mwokozi wetu.

Aidha Papa aliwakumbuka wafuasi wa Kanisa la Kiotodosi ambao kwa mujibu wa Kalenda yao ya Kiliturujia Jumapili hii ilikuwa ni Siku Kuu ya Pentecoste, na hivyo aliwaombea zawadi ya Roho Mtakatifu iwasaidie wote na hasa Mapatriaki,  Maaskofu wakuu na Maaskofu wanaounganika katika umoja wa Baraza lao . Papa alieleza na kuwaalika wote kuungana na Waotodosi kutolea sala kwa Mama Maria kwa ajili ya ndugu zetu hawa Waotodosi.

Pia aliitaja Jumatatu, amba yo niSiku ya Dunia ya Wakimbizi, kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa, ambayo kwa mwaka huu inaongozwa na Kaulimbiu: Kwa pamoja na Wakimbizi ni sehemu ya wale wanaolazimishwa kukimbia. Papa alikumbusha kwamba wakimbizi ni watu wa kawaida kama sisi sote , ni vile vita na ghasia zinavyoharibu makazi yao, kazi zao , jamii zao, marafiki wao n.k. , kama jinsi simulizi za maisha yao zinavyo gusa dhimiri zetu na kutoa  wito kweu sote wa kujenga amani katika haki. Hivyo Papa aliomba moyo wa kupenda kuwa pamoja nao, kukutana nao, kuwakaribisha, kuwasikiliza, na katika kuwa sehemu ya wapatanishi katika utiifu wa  mapenzi ya Mungu.

Papa alifunga kwa kutoa salam zake kwa mahujaji na wageni kutoka maeneo mbalimbali ya dunia, kikiwemo kikundi cha Wapanda Baiskeri wa Italia ACRA . 








All the contents on this site are copyrighted ©.