2016-06-13 16:03:00

Papa Francisko asikitishwa na mauaji huko Marekani!


Baba Mtakatifu Francisko amesikitishwa sana na mauaji ya kinyama yaliyopelekea watu 50 kupoteza maisha yao huko Orlando, nchini Marekani na wengine wengi kupata majereha makubwa kutokana na chuki zisizokuwa na sababu msingi. Baba Mtakatifu anaungana kwa njia ya sala na wale wote walioguswa na kutikiswa na msiba huu mzito, ili waweze kupata faraja kutoka kwa Mwenyezi Mungu.

Ni matumaini ya Baba Mtakatifu kwamba, vyombo husika vitaweza kubainisha sababu iliyopelekea mauaji haya ya kinyama ambayo inahatarisha hamu ya watu kutaka kuishi kwa amani na utulivu huko Marekani na sehemu mbali mbali za dunia. Maelezo haya yametolewa na Padre Federico Lombardi, Msemaji mkuu wa Vatican kwa niaba ya Baba Mtakatifu Francisko.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S.

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican.








All the contents on this site are copyrighted ©.