Mafundisho ya Baba Mtakatifu Francisko kwa mahujaji na wageni kwa Jumatano hii, yametazama kwa kina hoja mbili :umaskini na huruma ya Mungu. Ametoa tafakari kwa maisha ya watu wawili, mtu tajiri na maskini Lazaro, walioishi maisha tofauti kabisa katika mizania ya maisha, na kusema kumpuuza mtu maskini ni kumdharau Mungu, na kwamba Huruma ya Bwana kwetu inakiungo thabiti na sisi kuwa na huruma kwa wengine.
Papa alinukuu kama ilivyoandikwa katika Injili ya Matayo , Maskini Lazaro daima alipenda kulala mbele ya lango kuu la nyumba ya tajiri, akitamani hata kula makombo ya chakula yaliyokuwa ya kidondoka kutoka meza ya tajiri . Tajiri alivaa nguo anasa, wakati Lazaro alijifunika mwili wake uliokuwa umejaa vidonda kwa matambara yaliyochokaa. Tajiri kila siku alikula na kusaza wakati lazaro akifa kwa njaa , wala hakuwa na mtu wa kuhudumia madonda yake badala yake mbwa walikuja kulamba madonda yake .
Baba Mtakaifu amesema, mfano huu wa Lazaro na tajiri , unatukumbusha maneno makali ya ujio wa pili wa Yesu , ambamo alisema siku ya mwisho wa hukumu , Mwana wa Mtu atakapokuja tena kuwachukua walio wake na wasio wake atawaambia ”Mimi nilikuwa na njaa hamkunipa chakula, nilikuwa na kiu nanyi hamkunipa maji, nilikuwa [...] uchi hamkunivika " ( mt 25.42-43)”.
Papa anasema mfano wa maisha ya watu hawa wawili unatonyesha kwamba , Lazaro anawakilisha vizuri kilio cha kimya kimya cha baadhi ya maskini wa wakati wote na hali tata za ulimwengu ambamo utajiri mkubwa wa rasilimali za dunia umeshikwa na mikono ya wachache.
Papa ameendelea kueleza ilivyokuwa kwa watu hawa wawili Lazaro na Tajiri walipokufa . Tunasoma kwamba kukawa na mageuzi makubwa , aliyekuwa maskini anakuwa tajiri na tajiri anakuwa maskini. Lazaro anapa kutuzwa mbele ya uso wa Mungu na kuchuliwa na malaika na kulazwa katika kifua cha baba wa Imani Abraham .
Wakati mtu tajiri, alyeijiona amejitosheleza mwenyewe hapa duniani na kudharau ya Mungu , sasa anatupwa jehanamu katika mateso makali ya njaa akitamani hata tone la maji lidondoke ulimini mwake, kutuliza kiu yake . Lakini Abraham anamweleza kwa jinsi gani , utendaji wa haki na huruma inavyokuwa kutimiza fumbo Takatifu la Mungu linavyohusiana na husiana na matendo ya huruma na kwa wengine .
Papa aliendelea kuonya kwamba, kama ilivyokuwa kwa mtu huyo tajiri, milango ya mbingu imefungwa kwa wale ambao mioyo yao haiguswi na mahitaji ya watu maskini. Baada kifo na kutupwa jehananu mtu huyu tajiri ndipo anayafungua macho yake na kumwona Lazaro uwinginimikononi mwa Abrahamu. Tajiri huyo anajaribu kuomba msaada lakini anaambiwa amachelewa . Hivyo kumbe Papa anasema wakati ni huu wa wa wogofu , wakati wa kufungua mioyo na kuuona ukweli wa neno la Mungu na ujumbe wake wa kuokoa , kama alivyoimba Mama Yetu Bikira Maria katika wimbo wake mkuu . Ni kufanya mabadiliko katika maisha ya dunia hii kwa ushindi wa haki na huruma ya Mungu. Na wogofu wetu tusiuegemeze katiak miujiza , bali tufungue mioyo yetu wai kwa neno la Mungu anayetutaka tumpende yeye na jirani zetu.
BabaMtaktifu alikamilisha Katekesi yake kwa maneno kwamba, Neno la Mungu lina nguvu ya kuuinua moyo uliopondeka na kuuponya upofu wake . Na kwamba Ujumbe wa Mungu wa una uwezo wa kuibadilisha sura ya dunia hii kwa ushindi wake wa haki na huruma.
All the contents on this site are copyrighted ©. |