2016-05-14 17:24:00

Katekesi ya Papa yazungumzia huruma yenyewe


Baba Mtakatifu Francisko, Jumamosi akiendelea kutoa Katekesi kwa ajili ya Jubilee ya Mwaka Mtakatifu wa Huruma, aliitafakari  huruma yenyewe, ambayo ni  kati ya vipaji saba vya Roho Mtakatifu. Alisema kwamba, mara tunaposikia neno hili, tunapata hisia ya unyenyekefu fulani wa kidini au huba  ndani mwetu wenye  mvuto wa  mkubwa  wa kuwaelekea wale  wanahitaji upendo zaidi au kuhurumiwa. 

Papa aliendelea kuitaja huruma kuwa ni  kielelezo cha upendo wa Mungu kwa viumbe wake kama ambavyo  mara nyingi  tunavyosoma katika Injili. Tunaiona huruma ya Yesu kwa watu wengi  waliokuwa katika  hali ya mateso, wagonjwa, wenye  mapepo, maskini  na wanaoonewa ,  Yesu anajali mahitaji yao na kutoa jibu kwa  huruma na upendo . Walimgeukia Yesu wakiomba huruma yake “ Bwana Nirehemu”  (taz 10.47-48; Mt 15,22; 17,15)”. Yesu aliwatazama kwa huruma nao walipata faraja ya uwepo wake. Yesu aliwahimiza wamwamini Yeye na Neno lake , na alifanya miujiza ya uponyaji.

Kwa maelezo hayo Papa alitoa mwaliko kwa wote akisema  kuwa  sote tunatakiwa  kumuiga Bwana wa huruma  katika kusikiliza kilio cha wale wanaomlilia kutokana na  kutofautiana  kwetu  au wale waliotengwa kwa udhaifu wao. Sote tunatakiwa  kukujali  mahitaji ya ndugu zetu walio katika matatizo na mateso iwe kiwili au kiroho. Papa alikamilisha katekesi yake akiomba msaada wa  Bikira Maria, Mama wa huruma, Mfano wa mtu mwenye huruma,  atuwezeshe kupata neema ya kuuishi Jubilee hii ya mwaka wa  Huruma kwa kupata ukomavu zaidi katika  huruma na upendo kwa wote kwa kuiiga huruma isiyokuwa na kifani ya mwana wake Yesu Kristo.

Baada ya Katekesi yake , Papa alisalimia kw akutaja makundi mbalimbali ya watu waliofika kumsikiliza. Kati yao walikuwa wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Shirika la Mama Asiyekuwa na Ndoa, Pia Jumuiya ya Kipapa ya Mtakatifu  Josaphat ya Ukraina, na washiriki wa  kozi  ya majiundo ya wakufunzi katika  Chuo Kikuu Salesian. Pia  Wanachama wa Chianti, wakiongozwa na Askofu Giovannetti., Shirikisho Katoliki kwa ajili ya ufadhil  na wanachama Unitalsim na mahujaji wengi waliotoka Ufilipino na Uingereza na pande mbalimbali za dunia. Kwao wote Papa Frncisko ameonyesha matumaini yake kwamba,  Jubilee ya huruma, pamoja na kupita katika  Mlango Mtakatifu, inatoa  fursa ya kufikisha kwa ndugu zetu huruma  ya  Mungu Baba, kwa wale wote wenye kuhitaji  faraja katika shida zao.

Pia aliwasalimu  vijana, wagonjwa na Maarusi wapya. Na aliwakumbusha kwmaba,  Jumamosi hii ni sikukuu ya Mtakatifu Matthias, mtume wa mwisho kujiunga katika kundi la mitume  kumi na wawili. Alisema  nguvu yake ya kiroho, inawataka wapendwa  vijana, hasa wanafunzi katiak Chuo  cha Moyo Mtakatifu,  na Chuo cha  Paul VI cha hapa Roma, kuwa thabiti  katika imani yao katika kutelekeza kazi za  Bwana Mfufuka . Papa aliomba  msaada wa Bwana uwagemeza katika huduma yao  kwa wapendwa wagonjwa, katika nyakati za shida; na kujituma  kwao kwenye  utume wa kimisionari. Na aliwageukia wanadoa wapya akiwataka wakumbuke daima kwamba , upendo wao ni msingi  katiika kuiunganisha  familia.








All the contents on this site are copyrighted ©.