2016-05-03 09:16:00

Mapadri Wamercedari waaswa :Ni lazima kuwaendea waliosahaulika vitongojini


Mjumbe wa Mungu  huwa na mbinu za kuwafika watu maskini na kuwaweka huru dhidi ya matatizo yao, kwa kuwa amejawa na  Roho Mtakatifu,  mwanga na upepo wa nguvu wenye kutoa nguvu katika  dhamira ya uinjilishaji.  Ni ujumbe wa Papa  Francisko kwa Kundi la Mapadre wa Shirika la Wamercedari  waliomtembelea siku ya Jumatatu, mjini Vatican, kama sehemu ya Mkutano wao Mkuu wa nwaka na adhimisho la miaka kutimia miaka mia nane ya Shirika.

Katika hotuba yake fupi kwa Mapadri hao alionya dhidi ya majigambo kwa  sifa nzuri za nyuma,  bila ya kuwa na juhudi mpya zinazoendana na sura halisi ya nyakati hizi  ambamo mnahitajika  zaidi kuwa na njia mpya ya kutembeana katika njia ya  karama , kufanikisaha  haki, ukarabati wa makosa yaliyofanyika , na kujipa moyo na  kuwa na msukumo mpya wa kufanya hivyo katika maisha ya kileo.

Aidha Papa alikitazama kipindi hiki cha miaka mia nane ya Shirika na kusema kwa hakika ni mingi . Kwa ajili hiyo,  Papa Francisco  atongoza Ibada ya Misa kwa kushirikiana na kundi la Mapadre hao wapatao 50 wanaoshiriki katika Mkutano wao Mkuu na baadaye atawapokea katika Ukumbi wa Makardinali ulioko katika jengo la Kitume ndani ya Vatican. Mkutano Mkuu wa Shirika unaogozwa na Mada Mbiu: Wamercede: “kumbukumbu na unabii katika mazingira  uhuru”. 

Akionyesha kufurahia jina la Mkutano Mkuu, Papa  Francisko,  alisema kweli ni jambo jema kukumbuka  kazi kubwa iliyofanyika katika miaka hii mia nane ya Shirika. Lakini kumbukumbu hiyo isitie ujinga wa kubaki kujivunia tu yaliyofanyika katika kipindi hicho,  bali ni lazima yaliyofanyika yatumike kama kioo katika utendaji  wa wazi na ufahamu wa kujua wapi panahitajika kurekebishwa au kuongezewaa nguvu au palipo sahaulika, lakini  bila ya kwenda nje ya  mipaka ya shirika na hasa katika kukabiliana na changamoto  zinazogandamiza ubinadamu.  Ni muhimu kwa shirika kutafuta mbinu mpya za maisha  ya shirika kwa ajili ya  kuendelea kukabiliana changangamo za leo  na kuvumbua  majibu yenye huduma kwa  mahitaji halisi ya dunia na ya Kanisa, na wakati huohuo,  kubaki aminifu katika  urithi wa kudumu uliachwa na wahenga waanzilishi wa Shirikaa, urithi unaopaswa kutunzwa kama lulu kuu ya shirika

Aidha Papa aliwaambia kwamba,  ujuzi wao katika  kidini ni zawadi na uwajibikaji mkuu wenye thamani sana. Hata hivyo, Papa aliasa  juhudi si  zao binafsi,  lakini inatokana na kutegemea huruma ya Mungu daima ambayo ni nguvu na msaada kwa kila mmoja. Alisistiza  umakini na  uvumilivu katika sala na huduma ya hai ndani  na nje ya shirika. Ni kwa roho hiyo tu ,  kama unavyonena utangulizi wa kitabu chao cha Mwongozo”  Inawezekana  kuzungumzia  hali hali unabii, vinginevyo hatuwezi.  Papa  aliongeza  akisema, huu ni mwaliko kwa wale walioipokea zawadi ya Roho Mtakatifu kwa ajili ya kuwatumikia watu.  

Na kwamba "Nabii anajua anakotakiwa kwenda  vitongoji,  kuwakaribia watu na kuwaweka huru  dhidi ya mizigo yao inayowalemea”. Na  kinachomsukumu kufanya hivyo ni  Roho Mtakatifu anayevuvia  mwanga  wa njia ya kutembea na kuwasukuma mbele katika utendaji wao wenye kuhimiza kutembea katika nyayo za watangulizi wao,  Wahenga wao walioweza  kubaki katika maishaya dhiki  kama mateka na maskini, na watu waliotengwa katika jamii,  kwa nia ya kuwafariji  watu wanaokabiliwa na hali ngumu ya maisha kama hayo., wakichangia katika maisha ya  kila siku, siku moja baada ya nyingine,  hali ya  uvumilivu na ukimya wa maishayaliyo  huru na ukarimu, kwa manufaa ya wengine.   Papa alieleza na kukukumbusha juu ya utume wao wa  kuwakomboa maskini  wa maskini kwa kufungamana nao  na kuwatangazia habari njema hasa katika mwaka huu wa Huruma ili wote waweze kupeleka ujumbe huu.

Alihimiza , Ni kuwafikia wale wanaoteswa kwa sababu ya imani yao na wafungwa, waathirika wa biashara haramu,  vijana mashuleni, na wote wale wanaosubiri matendo ya huruma ya waamini katika Parokia , na wale wote waliokabidhiwa kwao na Kanisa. 








All the contents on this site are copyrighted ©.