2016-05-02 15:56:00

Papa kwa mara nyingine tena aomba amani Syria


Jumapili , Papa Fransciko akihutubia makumi ya maelfu ya watu waliokusanyika katika uwanja wa Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro hapa Vatican , baada ya sala ya Malaika wa Mbingu,  alionyesha hisia zake za dhati , zenye simanzi na uchungu mkubwa unaoletwa na maovu ya kujirudia mara kwa mara katika ghasia zinazoendelea Syria  bila kujali hadhi ya binadamu . Kwa ajili hiyo, Papa alirudia kutoa wito wa amanI nchini Syria akizitaka pande zote zinazohusika katika mzozo huu kuheshimu wito wa kusitisha ghasia za mapigano mara moja .

Papa kwa namna ya kipekee alilejea hali halisi hasa katika mji wa Aleppo, ambako watu wasiokuwa na hatia wanaendelea kuwa kafara wa vita hiyo , kati yao wakiwemo hata watoto wadogo na wagonjwa  na wale ambao wameyatolea maisha yao hata  kwa  gharama ya  maisha kuwa kuwa  sadaka, lakini hawarudi nyuma bali wanasonga mbele kupeleka  misaada  kwa  wanaohitaji.

 Papa alieleza na kuwatia moyo, wanachama wa  chama Italia, kinachopambana na kila aina ya dhuluma kwa watoto, akitaja madhulumu k wa watoto ni  janga! Alisema inawezekana kuvumilia yote lakini si  unyanyasaji kwa watoto! Ni lazima watoto walindwe dhidi ya ukali  na maovu , na wale wanaofanya uovu  dhidi ya watoto , azima waadhibiwe vikali,  alisema na kukishukuru chama cha Italia kwa ajili ya kazi zake  za kujitolea.

Aidha Papa akiyakumbuka Maadhimsho ya Mei Mosi,  Siku ya Kimataifa ya Wafanyakazi, ambamo pia aliutaja  Mkutano wa Kimataifa  ulioitishwa na Baraza la Kipapa la Haki na Amani kwa kushirikiana na Shirika la Kazi Duniani ILO. Mkutano  uliofunguliwa rasmi Jumatatu hii  mjini Roma,  juu ya mada: "Maendeleo Endelevu na  mifumo ya Kazi, katika  mazingira ya Jubilee wa Huruma".

Papa alionyesha matumaini yake kwamba, Mkutano huu , utaweza hamasisha  mamlaka na taasisi za kisiasa na kiuchumi na vyama vya kiraia, kukuza mfumo wa maendeleo endelevu  na kulinda  heshima ya utu wa mtu katika asjira na kazi. Aidha aliutumia muda huo kutoa salaam zake za matashi mema kwa Makanisa ya Mashariki ambayo yalikuwa yakiadhimisha Siku Kuu ya  Pasaka. Aliomba  Bwana aliyefufuka ,amimine zawadi ya mwanga  wake wa  amani kwa wote.

Awali kabla ya sala ya Malaika wa Bwana, Papa kwa Kifupi, alirejea somo la Injili ya Jumapili, lililopeleka mawazo ya waamini katika tukio la Karamu ya mwisho ya Bwana , kabla ya mateso na kifo chake Msalabani. Katika Karamu hiyo Yesu aliwaahidi mitume wake zawadi ya Roho Mtakatifu , atakayekuja kuwafundisha na kuwakumbusha maneno yake. Papa alisema, kumbe Kazi ya Roho Mtakatifu aliyemiminwa mioyo mwetu, wakati wa ubatizo na kipaimara,  ana kazi ya kutufundisha na kutukumbusha tunayopaswa kufanywa.

Alisema n akurejea Injili ya Yohane ,  ambamo Yesu anaeleza juu ya  Msaidizi, Roho Mtakatifu, atakayetumwa na Mungu kwa jina lake, ambaye atakuwa na kazi ya kufundisha kila jambo na kuwakumbusha yote aliyosema Yn 14:26. Na hivyo kumbe, kama waaamini hatuko peke yetu , Yesu yu karibu na sisi yu kati ya wafuasi wake yumo ndani mwetu. Uwepo wake mpya katika historia za maisha yetu naofanywa na Roho Mtakatifu, unakuwa ni njia ya kukarabati upya uhusiano wetu katika maisha ya pamoja na nae Yeye aliyesulubiwa na kufa  msalabani na Kuufuka. Roho Mtakatifu huingia upya ndani mwetu kupitia sakramenti za Kanisa , Ubatizo na Kipaimara. Ni yeye anayetuongoza katika namna za kufikiri na kutenda , katika kutambua kati ya mazuri na mabaya na hutusiadia kutenda kwa huruma ya Yesu , kujitoa sadaka kwa ajili ya wengine , na hasa kwa wanaohitaji zaidi msaada wetu. Papa aliomba zawadi hii ya  Roho Mtakatifu,  katika  Mwaka  huu Mtakakatifu Jubilei ya huruma, amkumbushe kila mtu kwamba,  ubinadamu wa  Yesu Kristo na Injili yake ni dhihirisho wazi la huruma ya Mungu.

 

 








All the contents on this site are copyrighted ©.