2016-04-23 09:18:00

Vita na fujo za kila siku ni kukataa maendeleo endelevu .


Kardinali Peter Turkson, Rais wa Baraza la Kipapa kwa ajili ya Haki na amani ,  Alhamisi iliyopita , mjini New York, akitoa mchango wa Jimbo la Papa katika Kikao cha ngazi ya juu kilichojadili Malengo ya Maendelea  Endelevu (SDGs ) ambayo dira ya utendaji wa serikali zote duniani katika kipindi cha miaka kumi na mitano ijayo yaani hadi 2030, alikumbusha kwamba, ufanikisha wa ajenda hiyo , si  ufadhili na fedha  tu katika mipango ya umma.  Lakini pia inahitaji  juhudi  msingi binafsi kama nyongeza muhimu ya kusaidia fedha zinazotolewa na serikali  kwa ajili ya mipango ya umma. Kwa hakika, ni muhimu kwamba Watendaji Wasio wa Kiserikali, kama vile vikundi vya kidini, asasi za kujitegemea na  ushirikiano wa  wadau mbalimbali katika uadilifu wa  shughuli  za kifedha, huondoa ukosefuw a usawa  wa kijamii na huendeleza mipango mipya iliyobora zaidi  kwa ajili ya ufanikishaji huduma za kawaida nzuri kwa wote.

Kardinali Turkson alieleza hilo baada ya kutoa salaam za Baba Mtakatifu Francisko , ambaye mwaka Septemba 25, 2015,  wakati  akilihutubia Baraza la Umoja wa Mataifa mjini New York ,  aliirejea ajenda ya Maendeleo endelevu ya hadi 2030, akiitaja kuwa ishara ya matumaini .  Hata hivyo alionya tumaini hilo linaweza tu kutoa matunda iwapo ajenda zitatendeka katika njia  ya  ukweli, haki na ufanisi ,  na muhimu zaidi , iwapo mfumo wake  utakuwa  endelevu. Hivyo ufanikishaji wa ajenda hiyo, unatoa wito kwa  wadau wote kutenda  kwa ufanisi kazi zote kwa moyo mmoja unaovutiwa kupenda kufanya hivyo. .

Kardinali Turkson aliendelea kuurejesha mkutano katika Waraka wa Papa Francisko juu ya utunzaji bora wa mazingira nyumba ya wote “Laudato si”, ambamo Papa amezungumzia  "huduma" na "kujali mazingira na maumbile ya dunia yetu kama nyumbani kwa viumbe wote. Na kwamba pale mtu anapojali , huonyesha mshikamano na wengine na hivyo huhusika na kuguswa na kinachoendelea.  Na katika kujali kutunza  yale yanayomzunguka,  mtu  pia huonyesha jinsi anavyo athiriwa na  mwingine asiyejali , kiasi kwamba  mipango  na vipaumbele  vyake huweza badilika ili alinde dhamira yake.  Hivyo katika  kujali, ugumu uliopo kati ya mtu binafsi na wengine hulainishwa, na pengine hata hutoweka.  Na hivyo basi pale tunapoamua kutupilia mbali chochocte kilicho chema,  tunaharibu sehemu yetu wenyewe kwa sababu  sisi  sote tumeshimanishwa katika kiungo kimoja.

Kardinali Turkison ameasa  kwamba,  ili kufanikisha ajenda  ya Maendeleo ya 2030,  tumetakiwa  kutunza mazuri yote yaliyopo , hata wakati  tunapotafuta  kuinua uchumi na fedha. Kukosa uwajibikaji wa Kimaadili katika mipango ya kuinua uchumi na fedha huzaa  tofauti  katika jamii. Kwa kutunza  vyema yaliyopo, tunavuviwa kutenda kwa kuwajibika katika  mipango yote ya kuinua uchumi na fedha na katika kukuza uwekezaji unaotakiwa kufanyika katika  malengo  ya  2030.

Mwisho wa hotuba yake, Kardinali Turkson aligusia umuhimu wa uwepo wa amani, kama ilivyotajwa na a Papa Paulo VI  katika Waraka wake wa Kitume wa mwaka  1967, juu ya Maendeleo ya Watu "Populorum Progressio,ambamo alisema  “maendeleo ni jina jipya la amani”. Amani ni sharti  na mazingira muhimu  na ya lazima  kwa ajili ya maendeleo yoyote ya kweli na ya kudumu. Kwa jinsi ilivyo kwa wakati huu ambamo dunia yetu imemezwa na uwepo  migogoro mingi ya kivita,  ukosefu wa amani, pengine inakuwa  changamoto kubwa zaidi katika kufanikisha malengo ya 2030.  Amani na huduma  ni vipengere  msingi zaidi katika kufanikisha maendeleo endelevu kuliko hata uwepo wa fedha na ufadhili.

Jimbo la Papa linasema , uwepo wa vita  na ghasia ni kukanusha ya haki zote na maendeleo  ya wote. Na hivyo linaasa,  utawala bora na vyombo vyote vya kisiasa kwa ajili ya udumishaji wa amani na usalama wa wote, vina umuhimu wa kipekee  katika ufanikishaji wa malengo ya  2030. 








All the contents on this site are copyrighted ©.