Wakristo wanatakiwa daima kuyakumbuka mambo mema aliyowatendea Mungu katika maisha yao, kwa kuwa , kufanya hivyo , huonyesha uimara katika kuifuata njia ya Imani. Papa Francisko alieleza Alhamis asubuhi, wakati wa Ibada ya Misa aliyoiongoza katika Kanisa dogo la Mtakatifu Vatican. Papa aliielezea Imani kuwa ni safari tunayoifanya katika maisha yetu ya kila siku kuelekea kwa Mungu. Hivyo ni jambo jema na lazima mara kwa mara kuyakumbuka yote Mungu aliyotufanyika katika hija hii, yaliyo mazuri. na pia majaribu na matatizo kwa sababu, Mungu kutembea na sisi, hakuondoi udhaifu wetu wa kibinadamu.
Papa katika homilía hii alifanya rejea kwa Mtume Paulo, wakati alipoingia katika Sinagogi la Antiokia na kuanza kutangaza habari njema ya Injili kwa kuwarejea kwa Wahenga wa Imani tangu Ibrahimu na Musa, Misri na Nchi ya Ahadi, mpaka kuja kwa Yesu. Papa aliyaita kwamba yalikuwa ni mahubiri ya kihistoria, yaliyotoa msingi muhimu wa imani kwa wafuasi wa Yesu , kwa sababu, Papa alisisitiza yanatukumbusha sote mambo muhimu, na ishara za uwepo wa Mungu katika maisha ya binadamu.
Papa aliendelea kutaja umuhimu kuyakumbuka ya nyuma, akirejea pia tukio la Alhamisi Kuu ambamo Yesu aliwaambia Mitume wake wakati wa karamu yake ya mwisho, kunyweni damu yangu na Kuleni mwili wangu kwa ukumbusho wangu. Na hivyo kwa kumbukumbu hii tunakumbushwa jinsi Mungu alivyotuokoa. Hivyo tunapaswa kuifanya kumbukumbu hii kwa moyo wa kina na uchaji , maana inatukumbusha jinsi Mungu alivyo tukomboa kwa upendo wake Mkuu, hadi kumtoa mwanae Msalabani .
Akasema, hivo ndiyo maana Kanisa linataka kila mara tushiriki katika kumbukumbu hii inayoadhimishwa katika Sakramenti ya Ekaristi, kama vile, ilivyokuwa kwa Wana wa Israel, ilivyoelezwa katika Kitabu cha Bibilia cha Kumbukumbu ya Torati. Sisi, pia, anasema Francis, ni lazima kufanya hivyo katika maisha yetu binafsi, kwa sababu kila mmoja wetu ametengeneza njia yake katika kumufuata Mungu , kutembea karibu na Mungu au katika kujiweka mbali na Bwana.
Papa alitaja umuhimu kufanya kumbukumbu hii katika ukweli toka ndani ya moyo na kutoa asante kwa Yesu, ambaye kamwe haachi kutembea pamoja nasi katika historia ya maisha yetu. Na akaonya, lakini bahati mbaya mara kwa mara katika udhaifu wetu wa kibinadamu tunaufunga mlango wa kiroho, tunamfungia Yesu nje, nje ya maisha yetu , na kupoteza imani kwake na hivyo tunakanusha wokovu aliotuletea. Lakini kwa kuyakumbuka ya nyuma , twaweza kujenga upya urafiki wetu na Yesu , na kuanza kutembea tena pamoja nae. Papa alieleza na kuhimiza kila mmoja wetu, daima kufanya kumbukumbu kwa mema mengi aliyotudea Mungu , tukiyaunganisha na matatizo na majaribu pia kwa kuwa vyote ni sehemu ya njia ya hija inayoelekea kwa Mungu.
All the contents on this site are copyrighted ©. |