2016-04-22 15:24:00

Jimbo la Papa lataja njia za kutokomeza tatizo la dawa za kulevya


Alhamisi 21 Aprili 2016, Askofu Mkuu Bernardito Auza , Mwakilishi wa Kudumu wa Vatican kwenye  Umoja wa Mataifa,  akitoa mchango wake katika Kikao maalum cha Baraza la Umoja wa Mataifa kilichojadili matatizo ya dawa za kulevya duniani , alikuwakumbusha wajumbe wa kikao hicho,  hotuba ya Papa Francisko,  kwa kikao cha Thelathini na Moja cha Mkutano wa Kimataifa juu ya Udhibiti wa Madawa,  ambamo Papa alisema kwamba, juhudi za kukabiliana na tatizo la  kuenea na ushawishi wa matumizi ya dawa za kulevya ,  haliwezi  kufikiwa kwa kulegeza masharti ya matumizi ya madawa hizo. Badala yake  ni muhimu,  kukabiliana na matatizo ya msingi yanayofanya hasa lika la vijana kujitoma katika dimbwi la ulevi wa dawa hizi kwa kukuza zaidi, haki, elimu, na maadili yanayohitaji kujenga maisha bora ya kijamii, pamoja na uwepo wa mipango ya kuandamana wanaoishi katika mazingira magumu na  shida, kuwapa njia zinazoweza  kuwapa matumaini ya kuwa na maisha mazuri  baadaye.

 Jimbo Takatifu linaona kwamba,  jaribio lolote, hata katika kiwango cha chini kabisa , lenye kutaka kuhalisha kile kinachoitwa dawa za burudani si tu uhalali wake kisheria unaleta  mashaka makubwa , lakini pia katika mtazamo wa athari zake kwa watumiaji.   

Zaidi ya hilo, Jimbo Takatifu linaongeza  kusema, vita dhidi ya dawa za kulevya haiwezi pata ushindi kwa kutumia dawa  kwa dawa na hasa kwa kuwa matumizi ya dwa za kulevya ni uovu , na uovu hauwezi jisalimisha  kwa maovu .  Na wala si tu kusema hapana kwa kila matumizi ya dawa za kulevya, bali wakati huohuo  wa kusema hapana ni muhimu na lazima kuwa na mbadala wa kusema  ndiyo katika maisha adilifu, ndiyo katika maisha ya  kuwapenda wengine , ndiyo katika elimu, na ndiyo  katika kutengeneza nafasi  nyingi za kazi. Linasema, “Tukisema 'ndiyo' kwa mambo yote haya, hapatakuwa na nafasi kwa vijana kujiingiza katika matumizi haramu ya  madawa haramu, wala  matumizi mabaya ya pombe, na aina nyingine za ulevi ulio nje ya uadilifu.

Jimbo la Papa limesisitiza hayo kwa kujingatia pia umuhimu wa kuwa na  familia thabiti asilia  kama kinga msingi, tiba, ukarabati kwa wale walio katika hatari za kuingia njia hii mbovu ya matumizi ya dawa za kulevya.  Mikakati thabiti ya maisha adilifu kwa familia  ndio msingi muhimu wa maisha ya kijamii, kama inavyodhihirishwa na tafiti zilizofanyika za sayansi ya kijamii,  juu ya maisha ya kijamii, kwamba, mwalimu na shule muhimu ya kwanza katika kanuni msingi za maisha ya mtu na kijamii, ni nyumbaniau  ndani ya familia. 

Hivyo, watoto ambao hulelewa katika  mazingira ya familia kwa ujumla, hupata  elimu muhimu  ya kuwasidia kusema "hapana" kwa matumizi haramu ya madawa  ya kulevya. Hivyo, elimu kwa watoto na vijana juu ya madhara ya madawa ya kulevya kinakuwa ni moja ya kipengele muhimu katika mapambano dhidi ya matumizi ya madawa  ya kulevya  na vishawishi vyake.

Ndani ya familia, kama ilivyo kwa jamii ,  kunahitajika mahusiano imara kwa ajili ya utulivu wa maisha na amani napia kuonyesha kuwasikitikia wale wanaoanguka  katika mitengo ya biashara haramu ya dawa ya kulevya na matumizi yake . Watu kama hao wanahitaji  msaada na huduma ya familia zao na jamii inayowazunguka .  Jimbo la Papa limeendelea kutazama uhalifu unaotokana na biashara haramu ya dawa za kulevya na matumizi yake likionya  pia kwamba,  kunahitajika utendaji wa haki sawa kwa wote wanaohusiak na tatizo hili tangu wale wanao fanyabiashara hiyo  Kimataifa  na wale ”pushers”  na watumiaji wenyewe, tofauti na ilivyo sasa, vyombo vya kisehria vikionekana kuwatia hatia zaidi watumiaji na wale wanaitwa pushers , ambako wahusika wakuu  kimataifa, mara nyingi hawaguswi .

Aidha Jimbo la Papa limeeelza tatizo jingine la biashara hii na  maovu yake yenye kuvuka mipaka,jinsi linavyo athiri  wananchi wengi  duniani kote, likitoa wito kwamba ni muhimu kuwa na  ushirikiano wa kimataifa, katika kujenga mwigiliano na mkakati jumuishi na wenye uwiano kwa ajili ya kupambana na uhalifu huu, kupitia kanuni  na sheria za jumuiya ya kimataifa zinazowalinda wananchi wote wa dunia kutoka na janga la dawa za kulevya.








All the contents on this site are copyrighted ©.