Baba Mtakatifu Francisko, akiendelea na mfululizo wa mafundisho yake juu ya huruma ya Mungu katika kipindi hiki cha Jubilee ya Mwaka Mtakatifu wa Huruma, Katekesi yake kwa Mahujaji na wageni, Jumatano hii, imevuviwa na Injili ya Luka ,mnamo onyesha huruma ya Mungu kwa mwanamke mdhambi aliyeingia nyumbani kwa Mfarisayo aitwaye Simoni. Mwanamke aliyejulikana kama mdhambi, anaingia nyumbani kwa Simoni na kuaguka miguuni pa Yesu na kuugua kilio kwa machozi mengi aliyoyakausha kwa nywele zake na kuibusubusu miguu ya Yesu na kuipaka mafuta ya marhamu ya bei ya juu.
Papa amelitafakari tukio hili akisema , akisema mna sura mbili, sura ya kwanza, unafiki wa Simoni Mwandishi na Mwanasheria, anayetazama dhambi za wengine na kuhukumu . Sura ya pili ni ya mwanamke, mdhambi anayeonyesha moyo wa majuto na unyenyekevu wa mtu mdhambi. Wakati Simoni anamhukumu mwanamke kwa matendo yake, licha ya kuwa mwenyeji wa Yesu, yeye hakuwa na wazo la kujipatanisha zaidi na Yesu au kuyashiriki maisha ya Bwana wake. Lakini mwanamke, anatenda kinyume, yeyé anaonyesha kujutia matendo yake , anaionyesha hali yake ya ndani kwa uwazi na kumwomba Yesu ayabadilishe maisha yake . NMwanamke anaonyesha imani yake kubwa kwa Yesu, upendo wa kweli na kamilifu na unyenyekevu, uliogusa huruma ya Mungu na kusamehewa dhambi zake.
Papa Francisko aliendelea kufafanua kwamba, Yesu hakunyanyapaa mwanamke mdhambi kwa kuwa alitofautisha kati ya dhambi na mdhambi. Hili linakuwa ni fundisho kwa Simon na sisi sote kwamba, hatupaswi kuwatenga wengine kwa sababu ya dhambi zao, kwa kuwa huruma ya Mungu hutolewa kwa watu wote wanaojutia dhambi zao na kuwa na imani kwa Mungu kama ilivyokuwa kwa mwanamke, kwa majuto na imani yake alisamehewa kusamehewa dhambi zake.
Papa alieleza na kuonya kuwa , tabia ya Simoni Mfarisayo, pia ipo kwetu . Daima tunataka kujiweka mbali na wadhambi ili tusije ambukizwa nao. Tuna wanyanyapaa wengine eti kwa sababu ni wadhambi. Lakini Yesu anamfundisha Simoni kutenda kinyume na mawazo hayo. Yesu anatufundisha kutofautisha kati ya dhambi na Mdhambi . Na kwamba hatupaswi kuikubali dhambi, lakini twaweza kuwa karibu na wenye dhambi, hasa kwa kuwa sisi sote ni wadhambi mbele ya Mungu. Sisi sote ni kama wagonjwa, tunaohitaji kuponywa na ili tupate kutibiwa kwanza tunahitaji kutambua maradhi yetu na kumweleza daktari. Tunahitaji kukutana na daktari wa Roho ambaye ni Yesu .
Yesu aliye Mtakatifu na Mungu, kwa huruma yake hakumzuia mwanamke mdhambi kujieleza kwa matendo. Anakubali kuguswa na mdhambi bila kumzuia au kuonyesha hofu ya kuchafuliwa nae. Yesu aliguswa na mwanamke akiwa huru kabisa , kwa sababu yu karibu na Mungu ambaye ni Baba mwenye Huruma. Katika ukaribu huu na Mungu, Baba mwenye huruma nyingi, Yesu anatufundisha kuwapokea wadhambi kama hatua ya kwanza ya kusamehe na kujenga uhusiano mzuri na wengine badala ya kwuatenga mbali kama wakosefu. . Yesu alimwambia wmanamke "Umesamehewa dhambi zako" na hivyo .. mwanamke akaenda kwa amani. Bwana aliona usafi wa imani yake na anamwokoa na kutangaza mbele ya wote: "Imani yako imekuokoa" (mstari 50)..na hivyo kuwa tofauti na unafiki wa mwanasheria, anaye mhukumu mdhambi . Kwa mwanamke tunaona jinsi dhamiri yake safi, unyenyekevu na imani vinavyompa hadhi ya kusamehewa kwa huruma.
Papa alieleza na kuonya kwamba , ndivyo ilivyo kwetu sisi, wote ni wenye dhambi, lakini mara nyingi tunaanguka katika majaribu ya kuwa wanafiki, kujiona sisi ni bora kuliko wengine. Hatupaswi kuangalia dhambi za wengine ili kutazama dhambi zetu wenyewe . Kutazama maporomoko yetu, makosa yetu na kumlilia Bwana. Somo hili la Injili lenye aya za wokovu zinatuonyesha jinsi ya kujenga uhusiano kati ya "mimI" mwenye dhambi na Bwana. Kama Mtakatifu Paulo anavyotukumbusha: "Katika Kristo, kwa damu yake, tunao ukombozi, msamaha wa dhambi, sawasawa na wingi wa neema yake. Papa ameitaja kuwa ni zawadi ya imani, na hivyo tunapaswa kumshukuru Bwana kwa upendo wake mkuu ambao hatuna mastahili ya kuupata. Tunapaswa kushukuru kwa upendo huu uliomwangwa kwetu, juu ya ndugu zetu, katika nyumba zetu, katika familia zetu na , katika jamii , ambayo ni huruma yote ya Mungu kwetu.
All the contents on this site are copyrighted ©. |