2016-04-18 07:22:00

Mh. Padre Angelo Pagano ateuliwa kuwa Askofu wa Harar, Ethiopia!


Baba Mtakatifu Francisko amekubali ombi la kung’atuka kutoka madarakani lililowasilishwa kwake na Askofu Woldetensaè Ghebreghiorghis wa Jimbo la Kitume la Harar, nchini Ethiopia kadiri ya sheria za Kanisa namba 401 Ibara 1. Wakati huo huo, Baba Mtakatifu ameteua Mheshimiwa Padre Angelo Pagano kuwa Askofu mpya wa Jimbo la Kitume la Harar,nchini Ethiopia. Kabla ya uteuzi huu, Askofu mteule alikuwa Paroko na Mkurugenzi wa Miradi ya Wakapuchini nchini Cameroon.

Taarifa zinaonesha kwamba, Askofu mteule Angelo Pagano, O.F.M. Cap. alizaliwa tarehe 15 Januri 1954 huko Asmara, nchini Eritrea, wakati huo, sehemu hii ilikuwa bado ni eneo la Ethiopia. Baada ya masomo na majiundo yake katika masuala ya elimu dunia, akiwa na umri wa miaka 25 akajiunga na Shirika la Ndugu Wafrancisko Wakapuchini aliokuwa amewafahamu wakati walipokuwa wanaishi huko Asmara. Baada ya majiundo yake ya kitawa, akaweka nadhiri za daima kunako mwaka 1981.

Akapadrishwa tarehe 25 Juni 1988 na kupelekwa nchini Cameroon kama mmissionari. Tangu wakati huo, amekuwa Paroko msaidizi, Paroko na kuanzia mwaka 1988 hadi mwaka 2000 alikuwa ni Rais wa Baraza la Wakapuchini Afrika Magharibi. Kuanzia mwaka 1993 – 2000 Mwakilishi wa Wakapuchini na hatimaye, akateuliwa kuwa mwakilishi wa kwanza wa Wakapuchini, dhamana aliyopewa tena kunako mwak 1996 hadi mwaka 200. Kuanzia mwaka 1996 hadi mwaka 2003 alikuwa ni mwanachama wa Baraza la Wakleri Jimbo Katoliki la Kumbo.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S.

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican








All the contents on this site are copyrighted ©.