Baraza la Umoja wa Mataifa limeanza Mchakato wa kuchagua Katibu Mkuu mpya wa Umoja wa Mataifa, kwa kusikiliza maoni na utetezi wa wagombea kiti hicho kinacho achwa wazi na Bwana Ban Ki moon anayemaliza muda wake mwishoni mwa mwaka huu. Taarifa ya Alhamsi imetaja uwepo wa wagombea tisa wa kiti hicho wanne wakiwa wanawake na watano wanaume. Majina ya wagombea ni :
Bi Vesna Pusic wa Croatia ambaye kwa wakati huu Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje na masuala ya Ulaya, na anagombea kwa tiketi ya nchi za Ulaya Mashariki.
Bwana Srgian Kerim wa Macedonia anagombea kwa tiketi ya nchi za Ulaya Mashariki
Bi Natalia Gherman wa Moldova ambaye ni Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano katika Umoja wa Ulaya anagombea kwa tiketi ya Nchi za Ulaya Mashariki EEG.
Bwana Igor Luksic wa Montenegro ambaye ni Waziri wa Mambo ya Nje, anagombea kwa tiketi ya EEG
Bi Helen Clack wa New Zealand ambaye kwa wakati huu ni Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa kwa ajili ya Mipango ya Maendeleo(UNDP) anagombea kwa tiketi ya Ulaya Magharibi.
Bwana Antonio Guterres wa Ureno Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa kwa ajili ya Wakimbizi(UNHCR) anagombea kwa tiketi ya Ulaya Magharibi.
Vuk Jeremio wa Serbia anagombea kwa tiketi ya Ulaya Mashariki
Danilo Turko wa Slovania kwa Tiketi ya Nchi za Mashariki (
Jumatano Danilo Turko, alitoa maoni yake juu ya uongozi wa Umoja wa Mataifa katika miaka mitano ijayo baada ya Ban, akisisitiza umuhimu wa kuimarisha ubia baina ya Umoja wa Mataifa na jumuiya za kikanda, asasi za kiraia, wafanya biashara, na vyombo vya habari ikienda sanjari na Kazi kuu tatu za Umoja wa Mataifa ambazo ni kudumisha amani na usalama, maendeleo endelevu na haki za binadamu.
Aidha Jumatano Mgombea Dkt. Vesna Pusić, alitoa maoni yaliyojikita zaidi katika usimamizi wa Malengo ya Umoja wa Mataifa. Alisema Umoja wa Mataifa usipofanya kazi nzuri ya kusimamia amani, maendeleo, misaada ya kibinadamu, haki za binadamu, miradi yote ya elimu na maendeleo, yote yatabaki kuwa ndoto tu za kufikirika . Ni lazima kuwa na usimamizi thabiti wenye kuhakikisha maamuzi yanayotolewa kweli yanatimizwa na nchi wanachama wa umoja huo.
Na Bi Natalia Gherman, kutoka Jamhuri ya Moldova,pia alitoa maoni yake , na alikazia zaidi suala la usalama, maendeleo na haki za binadamu, akisema "Hakuna usalama bila maendeleo, na hakuna maendeleo bila usalama, na hakuna lolote bila kuheshimu haki za binadamu. Na Umoja wa Mataifa ni lazima ujitahidi zaidi kutimiza ahadi zake juu ya ubia mpya wa kimataifa kwa manufaa ya wakazi wote wa dunia. Ni jukumu la Umoja wa Mataifa, kusaidia nchi wanachama kutimiza ahadi hizi. Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa Alhamisi limeendelea kuwasikiliza wagombea.
All the contents on this site are copyrighted ©. |