2016-04-09 10:05:00

Papa Francisko kutembelea Armenia, Juni; Georgia na Azerbaigian, Sept, 2016


Baba Mtakatifu Francisko amepokea kwa mikono miwili mwaliko kutoka kwa Patriaki Karekini II, Mkuu wa Kanisa la Waarmeni wote, viongozi wa Serikali pamoja na Kanisa kutoka Armenia na ameamua kutembelea nchini humo kuanzia tarehe 24- 26 Juni 2016.

Wakati huo huo, Baba Mtakatifu Francisko amepokea na kukubali mwaliko kutoka kwa Patriaki Ilia II wa Kanisa la Georgia, viongozi wa Serikali na wa Kidini wa Georgia na Azerbaigian. Baba Mtakatifu Francisko anatarajiwa kufanya hija hii ya kitume katika nchi hizi mbili kuanzia tarehe 30 Septemba hadi tarehe 2 Oktoba 2016. Baba Mtakatifu atahitisha hija yake ya kitume kwa kutembelea mji wa Caucaso.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S.

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican








All the contents on this site are copyrighted ©.