2016-04-08 10:06:00

Papa awaambia wadhamini kamwe wasichoke kutenda mema!


Ijumaa hii nyakati za adhuhuri , Baba Mtaktifu Francisko aliwapokea na kuzungumza nao , wajumbe kutoka Baraza la Wadhamini na mawakili wa Taasisi ya Kipapa ya Mfuko wa Mtakatifu Petro , kama sehemu ya hija yao ya kila mwaka mjini Vatican.  Papa aliitumia nafasi hiyo kutoa shukrani zake za dhati kw aukarimu wao wanao uonyesha kwake yeye binafsi na kwa Kanisa la ulimwengu akiomba wafikishe shukurani hizo kupitia kwao kwa wote wanaotembea katika njia hii ya ukarimu wenye kufanyika kazi zao za matendo mema.

Papa aliigeukia hija yao ya mwaka huu inayofanyika  katika kipindi cha  mwaka Mtakatifu wa Jubilee ya Huruma ,kiutaja kwamba ni  wakati wa kipekee wa  kutafakari fumbo la huruma, kama  chemchemi ya furaha, utulivu na amani katika  wokovu wa binadamu.  Na kwamba kama Wakristo wameitwa kuifikisha  huruma hii hasa kwa wale ambao  kiroho na kimwili wanahitaji  kwa njia za kiroho na  kazi za matendo ya huruma kupitia roho ya ukarimu na huruma kuonyesha wema na huruma ya Mungu isiyokuwa na kipimo.  

Kama Wajumbe, Wadhamini, na mawakili wa Taasisi ya Mfuko wa Papa, matendo ya huruma yanakuwa ni kiini katika moyo wa kazi zao. Kupitia msaada wa ukarimu kwa Jimbo, Parokia na Jumuiya za Kikristo, huwezesha ufanikisha wa miradi  na pia utoaji wa ufadhili katika masomo , na hivyo kuwa msaada kwa watu wengi kutoa jibu  chanya kaika mahitaji ya jumuiya mahalia na hivyo daima kuzaa matunda mengi  ya kazi za matendo ya huruma.  Kwa njia hiyo,  upendo wao hububujika  duniani kote, kama sadaka mpya katika  juhudi mpya ili kusaidia mpanuko wa kuikumbatia na huruma ya Baba.

Baba Mtakatifu ameomba  siku hizi za hija yao ziwape hamasa mpya katika  kuuishi Utakatifu,  na uzoefu walioupata kama zawadi ya huruma ya Mungu. Alieelza na kuwarejesha katika maneno ya Mtakatifu Paulo yanayokumbusha  kamwe kutochoka kutenda mema ( Gal 6: 9; 2 Thes 3:13). Aliwapa Baraka zake kwa kumwomba  Baba awategemeze katika matendo yao ya  mema, lakini juu ya yote  awaongozee imani na upendo wake usio na mwisho.  Na aliwaomba pia wasimsahau katika sala zao. 








All the contents on this site are copyrighted ©.