2016-04-06 14:42:00

Nia ya sala za Papa yawalenga wakulima wadogowadogo


Nia ya sala za Baba Mtakatifu kwa mwezi huu wa Aprili 2016 , inawalenga zaidi wakulima wadogowadogo na mahangaiko yao. Papa ameeleza nia yake kupitia mtandao wa video  wa dunia , ulioanzishwa kwa makusudi ya kutoa msaada katika kusambaza  nia  ya sala za kitume za Papa kwa  dunia nzima, hasa kwa changsamoto zinazopambana na uso wa dunia.

Katika ujumbe wake alioutoa kwa ajili ya Nia za Aprili, ,Baba Mtakatifu kwa dhati anashukuru juhudi za wakulima wadogowadogo, katika kufanikisha mahitaji muhimu kwa watu wote. Na pia  kwa  ajili ya kumjali kila  mtu binafsi kama Mtoto wa Mungu, anayestahili  maisha yenye heshima.  Lakini pia amehoji kwa mshangao, nani  hulipa  fidia ya kazi zao nzito za wakulima hawa? Pia Papa anaukumbusha uliwmengu kwamba, dunia  hii ni zawadi kutoka kwa Mungu. Na hivyo si haki kwa  rasilimali  zake kutumika kwa manufaa ya wachache, wenye kupokonya haki na  manufaa kwa walio wengi.

Papa ameeleza na kutoa mwaliko kwa watu wote kuongeza sauti zao katika sauti yake katika  nia hii sala, ili wakulima wafogowadogo waweze kupata fidia ya haki kwa kazi yao  ya thamani sana .

 








All the contents on this site are copyrighted ©.