2016-03-30 11:57:00

Wajumbe wa Tume ya Kipapa ya Biblia kuanza mkutano wao 4-8 Aprili 2016


Tume ya Kipapa ya Biblia, kuanzia tarehe 4 hadi 8 Aprili 2016 itakuwa na mkutano wake wa mwaka kwenye Hosteli ya Mtakatifu Martha, iliyoko mjini Vatican. Mkutano huu utakuwa chini ya usimamizi wa Kardinali Gerhard Ludwic Muller Rais wa Tume na Padre Pietro Bovati, SJ, Katibu mkuu wa Tume. Mkutano huu ni ufuatiliaji wa utekelezaji wa Waraka wa Tume hii uliochapishwa kunako mwaka 2014 na Kitengo cha Uchapaji cha Vatican, LEV.

Waraka huu unajulikana kama “Uvuvio wa Roho wa Mungu na Ukweli wa Biblia. Neno linalotoka kwa Mungu na linamzungumzia Mungu ili kuokoa ulimwengu”. Tume ya Kipapa ya Biblia imeanza kufanya tafakari za kina kuhusu tema zenye mwono kuhusu elimu ya binadamu katika Biblia.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S.

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican.








All the contents on this site are copyrighted ©.