2016-03-23 15:16:00

Papa akemea mashambulio ya kigaidi


Baba Mtakatifu Francisko amekemea vikali mashambulio ya mabomu yaliyofanyika jijini Brussles Ubelgiji mapema Jumanne, akisema ni upuuzi mtupu.. Mashambulio hayo yalifanyika katika maeneo mawili  tofauti  katika uwanja wa ndege na katika kituo cha reli na kusababisha zaidi ya watu 30 kufariki dunia na wengine  230 kujeruhiwa. Katika telegram Papa iliyotiwa  saini na Katibu wa Vatican, Kardinali  Pietro Parolin, ameonyesha masikitiko ya Papa na  ukaribu  wake kwa wahanga kupitia sala zake kwa Marehemu na majeruhi na pia kwa jamaa zao, ambamo amemwomba Mungu zawadi ya amani.

Pia , Jumatano hii wakati wa Katekesi yake, Papa kwa huzuni aliwakumbuka wahanga wa mashambulio ya kigaidi yaliyofanyika Ubelgiji  n akuomba ushirikiano wa watu wote kupambana na unyama huu unaofanywa na magaidi. Kutokana na janga hili Serikali ya  Ubelgiji imetangaza siku tatu za  maombolezo ya kitaifa.  Taarifa toka Brussles inabaini kwamba, mabomu hayo yalikuwa yemeshehenezwa kwa misumari mikali, na kwamba  bomu jingine lilibaki bila kulipuka.

Kutokana na hali hiyo, uwanja wa ndege wa Zaventen ambako watu kumi walifariki ulifungwa kwa bomu lililolipuka majira ya saa mbili za asubuhi, ulibaki umefungwa hadi mapema asubuhi hii.. Polisi imetoa picha za watu watatu wanaotuhumiwa kuhusika na ulipuaji wa mabomu katika uwanja huo. Waziri Mkuu wa Ubelgiji Charles Michel na Kiongozi wa kijadi Mflame  Philip, kupitia njia ya televisheni wamewataka raia wa Ubelgiji kubaki  imara katika utulivu na utu, licha ya changamoto hii yenye kusababisha woga wa kutisha.

Nao Maaskofu wa Ubelgiji, baada ya kupata taarifa za shambulio hili, wametoa tamko lao la kichungaji, ambamo wameungana na jamii yote yenye mapenzi mema wanaoombeza msimba huu uliosaba bishwa na b inadamu kafiri katika uwanja wa ndege wa Zaventem na katikati ya Brussels. Wametolea Maombi yao na kuwakabidhi waathirika wote , katika huruma ya Mungu . Maaskofu pia wamefahamisha uwanjani, kuna makasisi kwa ajili ya kutoa huduma za kiroho kwa wanaohitaji.   Maaskofu walimalizia rambirambi zao kwa kwa kuwaomba raia wote wa Ubelgiji kukiishi kipindi hiki kigumu cha majaribu kwa kuziishi siku hizi na uwajibikaji mkubwa wa raia mwema.

Na Rais wa Baraza linalounganisha Mabaraza ya Maaskofu yote barani Ulaya(CCEE),  Kardinali Peter Erdo, ameyataja masikitiko ya Maaskofu wa Ubelgiji kwa paoja na  Baba Mtakatifu na  Maaskofu wa wote wa Ulaya. Kardinali Peter Erdo, pia ameyaita mashambulio hayo kuwa ni vitendo vya kinyama si tu vinazidisha hofu ba wasiwasi kwa watu wa Ulaya lakini duniani kote. Na hivyo amehimiza kutovujika moyo lakini kubaki imara  katika kuombea amani,  Ulaya, Mashariki ya Kati na duniani kote.  Na  Rais wa COMECE na Baraza la Maaskofu wa Ujerumani ', Kardinali. Reinhard Marx, pia tamko lake limeonyesha kushtushwa na kuhuzunishwa na  kile kilichotokea. Mara aliyapeleka mawazo yake na ukaribu wake kwa Marehemu na  waliojeruhiwa na jamaa zao, akisema katika Wiki hili Takatifu na  tuombee hasa kwa waathirika wa unyanyasaji na familia zao. Aidha ametaja ukaribu wake na wale wote wanaofanya kazi na Katibu wa COMECE ofisi za Ubelgiji. Na pia  amepeleka salaam zake za rambirambi kwa Maaskofu Ufaransa na  Askofu Mkuu wa Barcelona, ​​Msgr. Juan Jose Ornella, kufuatia matukio ya kusikitisha yaliyotokea hivi karibuni katika Jimbo kuu la Malines na Brucelles. 








All the contents on this site are copyrighted ©.