2016-03-22 14:29:00

Umoja, ubinadamu na kazi ni nguzo kuu katika kujenga amani na utulivu


Mtazamaji wa kudumu wa Jimbo la Papa katika Umoja wa Mataifa, na Baraza la Usalama , Askofu Mkuu Bernardito Auza, Jumatatu Machi 21, 2016,  alishiriki katika majadiliano yanayotafuta jibu la kukabiliana na kipeo cha mizozo na ghasia katika Ukanda wa Maziwa Makuu Afrika. Hotuba ya Askofu Mkuu Auza ilipongeza urais Angola kwa kurejesha mjadala huo unaolenga kutengeneza azimio kwa ajili ya kuzuia na kudhibiti Migogoro  ya kisiasa katika Ukanda wa Maziwa Makuu Afrika kwa ushiriki wa jumuiya ya kimataifa.

Na ilirejesha mawazo ya Papa Francisko wakati alipofanya ziara yake katika ukanda huo kunako mwezi Novemba mwaka jana,ambako alisisitiza kwa nguvu, kaulimbiu ya umoja na mshikamano , utu na kazi,  katika Jamhuri ya Afrika ya Kati, kama hatua ya kujinasua na tabia za ghasia na ulipizaji kisasi, akisema si tu katika taifa hilo lakini ni katika ukanda wote wa Afrika Kati na Ukanda wa Maziwa Makuu. Ukanda unaoendelea  kwa miongo kadhaa, kukabiliwa  na migogoro mbalimbali ya ndani ya nchi yenye  kuchochewa miongoni mwa mambo mengine, migogoro ya kisiasa na utawala mbovu, rushwa na umaskini uliokithiri, mgawanyiko wa kikabila na matumizi mabaya na unyonyaji wa rasilimali nyingi za asili za eneo hilo.

Ujumbe wa Jimbo la Papa ulionyesha imani yake kwamba, ni tu  mambo matatu ya  kimaadili yanayoweza maliza matatizo katika ukanda huo nayo nayo ni umoja, utu na kazi. Hizo ni nguzo za jamii yoyote kuwa na mafanikio .  Hiyo ni barabara inaweza kwa kiasi kikubwa kuwezesha ufumbuzi wa sababu tata za migogoro ya kivita na kukosekana kwa maendeleo katika Mkoa huo. Ameonya, . hakuna ufumbuzi unaoweza kupatikana kwa  matatizo mengi Mkoa huo, ikiwa kutaendelezwa  mgawanyiko badala ya umoja, ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu badala ya heshima kwa utu wa wote, na umaskini uliokithiri badala ya kazi zenye heshima kwa wote. Umoja ni nguzo ya  thamani kwa maelewano ya watu katika utofauti wao wote. Umoja huweka mbali  hofu nyingi za  makabila mengine na jamii.  Umoja hutambua wingi wa maoni ya kisiasa na imani za kidini.  Umoja ni humaliza rushwa na uchoyo vyenye kuhatarisha haki na mshikamano.

Askofu Mkuu Auza aliendelea kutafsiri thamani msingi ya umoja katika utofauti, akisema katika ukweli ni changamoto ya  mara kwa mara, yenye kuhitaji ubunifu, ukarimu, kujinyima na heshima kwa watu wengine. Kisha, kuheshimu hadhi ya mtu ni kuheshimiana wote,  na kuwa na mshikamano unaotoa uwezekano kwa kila  mtu kutambua asili na usawa  wa hadhi kwa  wote. Ni katika utambuzi kwamba wale wenye uwezo wa kufurahia maisha bora, badala ya kuwa na wasiwasi na marupurupu juu ya hali yao, wanapasea kutafuta mbinu za kutoa msaada kwa wahitaji zaidi katika  hali ya kuheshimu maisha ya wote. Alirejea tena hotuba ya Papa Francisko huko Bangui, ambamo alihimiza nchi zote katika Mkoa huo, zenyewe kufany akila bidii kuboresha maisha yaa kwa kutumia kwa busara rasilimali zao nyingi .

Pia Jumuiya ya kimataifa lazima kusaidia nchi ya Mkoa huo kuhakikisha kwamba utajairi hu owa rasilimali iwe kweli baraka badala ya kuwa balaa la. Iwe ni neema kwa wote badala ya kuwa upendeleo kwa wachache wanaonyonya wengine  na kuneema kwa migogo ya wote. Na ili hayo yafanyike kunahitajika utawala bora aminifu katika  mamlaka za umma. Jimbo la Papa limelaani vikali tamaa za kukimbilia silaha kunapojitokeza kutoelewana.








All the contents on this site are copyrighted ©.