2016-03-22 14:12:00

Papa ampokea hati za utambulizsho toka kwa Balozi mpya wa Indonesia


Jumatatu, Papa alimpokea Balozi mpya wa Indonesia katika Jimbo Takatifu , Balozi  Antonius Agus Sriyono. Katika tukio hili, Balozi Antonius, rasmi aliwasilisha hati zake za utambulisho kwa Papa kama pia ishara ya  kuzindua  mwanzo wa kazi zake katika Kiti  Kitakatifu.

Habari binafsi za Balozi Antonius zinasema, ni alihitimu masomo ya  mahusiano ya kimataifa katika Chuo Kikuu cha Gadjah Mada cha  Sriyono baadaye alichukua masomo ya kidiplomasia kabla ya kuanza kazi katika huduma za kidiplomasia. Baada ya hapo, alishika nyadhifa mbalimbali kadhaa katika Wizara ya Mambo ya Nchi za nje  ya Indonesia , pia  kutumikia katika  ofisi za ubalozi wa Indonesia huko Uholanzi, Umoja wa Mataifa na Urusi , kabla ya kuwa Balozi wa New Zealand, 2010-2013.

Sehemu kubwa ya raia wa Indonesia ni Waislamu wanaofkia zaidi ya asilimia  87% katika idadi ya  milioni 255, na hivyo ni kati ya mataifa za Kiislamu duniani.   Wakatoliki  ni asilimia % 2.8 tu ya wakazi wote. Jimbo Takatifu liliitambua Jamhuri ya Indonesia tangu mwaka 1947 na kuanzisha uhusiano wa kidiplomasia na taifa hilo. Na kunako mwaka 1950, Vatican ulipandisha  uwakilishi huo na kuwa ubalozi katika ngazi ya kimataifa ambamo mwaka 1965 ukawa Ubalozi kamili.  Taifa hilo ambalo liko Kusini Mashariki mwa Asia, limetembelewa na Mapapa Wawili,  Mwenye Heri Yohana  Paulo VI kunako mwaka 1970 na  Mtakatifu Yohana  Paul II mwaka 1989.








All the contents on this site are copyrighted ©.