2016-03-21 06:46:00

Papa asikitishwa na shambulizi la kigaidi nchini Uturuki!


Baba Mtakatifu Francisko katika ujumbe ulioandikwa kwa niaba yake na Kardinali Pietro Parolin, Katibu mkuu wa Vatican anapenda kuonesha mshikamano wake wa dhati na wananchi wa Uturuki walioguswa na shambulizi la kigaidi lililotokea huko Instanbul tarehe 19 Machi 2016 na kusababisha vifo vya watu 5 na wengine 36 kujeruhiwa vibaya.

Ujumbe wa Baba Mtakatifu umepelekwa kwa Rais Recep Tayyip Erdogàn wa Uturuki. Baba Mtakatifu anawaombea wananchi wote wa Uturuki kuwa na moyo mkuu pamoja na kuwaweka marehemu wote chini ya huruma ya Mungu! Anawaombea wale wote walioguswa na maafa haya nguvu, amani na faraja!

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S.

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican.








All the contents on this site are copyrighted ©.