2016-03-16 15:53:00

Amani kwanza Zanzibar!


Kufuatia hali ya Amani Zanzibar kuwa mashakani kutokana na mgawanyiko miongoni mwa jamii unaosababishwa na tofauti mbalimbali zikiwemo za kisiasa. Baraza la Viongozi wa Dini mbalimbali kwa Ujenzi wa Amani Tanzania (IRCPT)  wamewakutanisha viongozi wa Dini wa madhehebu mbalimbali ya Kikristo na Kiislam  pamoja na Jumuiya ya Kihindu kutoka Tanzania Bara na Visiwani kuzungumzia hali halisi Zanzibar na nini kifanyike kudumisha amani, ambao baada ya majadiliano ya kina wameazimia yafuatayo:

MAAZIMIO:  Kwa kutambua kuwa Zanzibar ni moja na watu wake ni wamoja na amani ni tunu adhimu kwa watanzania wote,

1. Viongozi wa Dini tunawapongeza Watanzania wenzetu wa Zanzibar kwa kuwa wavumilivu na kuilinda  Amani katika kipindi cha uchaguzi na baada ya uchaguzi hadi sasa.

2. Viongozi wa Dini, wajitenge na siasa za vyama, kwani wao wanapaswa kua nguzo za jamii zenye Imani na asili tofauti, wasuluhishi na watetezi wa Amani nchini

3. Vyomba vya usalama, wawabaini na kuwachukulia hatua vikundi vya uvunjifu wa Amani ili wananchi waishi kwa Amani. (Watumie nguvu inayostahili na isiogopeshe umma)

4. Vyama vya siasa vinavyotoa kauli n ataarifa zisizo sahihi na kuleta uchochezi. Viache mwenendo huo ili kudumisha Amani. Kwani kila mmoja ana wajibu wa kuiteteaTunu hii yaTaifa.

5. Tume ya Uchaguzi, wawe waadilifu, kusimamia haki, sheria, kanuninauwaziilikudumisha Amani katikakipindihiki cha uchaguzi

6. Vyombovyahabarivisaidiekuhakikishatunapitakwenyeuchaguzikwausalamanaamanikwakutoataarifasahihi, kuzingatia maadili na kufuata taratibu na sheria zilizopo.

7. Mahali ambapo uvunjifu wa Amani na wahusika nidhahiri vyombo vya usalama wachukuliwe hatua stahiki za kisheria.

8. Wananchi ambao pia ni waamini wetu wailinde Amani kutoka mioyoni mwao, kwani ni wajibu wao wakiroho na kijamii.

9. Wananchi watakaoshiriki kupiga kura wakitumia haki yao ya kimsingi, wahakikishiwe Amani na wale ambao hawatashiriki wasibugudhiwe na wao pia wahakikishiwe Amani.  “Zanzibar moja, watu wake ni wamoja, tuungane kulinda amani kwa maendeleo yetu” “Amani kwanza”

 








All the contents on this site are copyrighted ©.