2016-03-15 15:39:00

Kanisa kupata watakatifu wapya watano!


Baba Mtakatifu Francisko, Jumanne tarehe 15 Machi 2016 ameongoza Sala ya Kanisa na katika mkutano huu wa kawaida wa Makardinali amepitisha majina matano ya wenyeheri watakaotangazwa kuwa watakatifu wakati huu wa maadhimisho ya Mwaka Mtakatifu wa Jubilei ya huruma ya Mungu. Wenyeheri watakaotangazwa kuwa watakatifu hapo tarehe 5 Juni 2016, Jumapili ya X ya Kipindi cha Mwaka wa Kanisa ni Stanslaus wa Yesu wa Maria na Mwenyeheri Maria Elizabeth Hesselblad.

Kanisa litamtangaza Mama Theresa wa Calcutta kuwa Mtakatifu, Jumapili tarehe 4 Septemba 2016. Wenyeheri Giuseppe Sànchez wa Rio na Giuseppe Gabriele wa Rozari Takatifu Brochero watangazwa kuwa watakatifu tarehe 16 Oktoba 2016. Hawa ni kati ya wenyeheri walioshuhudia huruma na upendo wa Mungu katika maisha yao, sasa wanatangazwa na Mama Kanisa kuwa ni mashuhuda na vyombo vya huruma ya Mungu, mfano bora wa kuigwa!

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S.

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican.








All the contents on this site are copyrighted ©.