2016-03-14 14:48:00

Papa Francisko asikitishwa na mauaji ya wananchi huko Ankara, Uturuki!


Baba Mtakatifu Francisko amesikitishwa na taarifa za mauaji ya watu 34 yaliyotokea huko Ankara, Uturuki Jumapili tarehe 13 Machi 2016 na wengine 125 kujeruhiwa vibaya kutokana na mashambulizi ya kigaidi. Baba Mtakatifu anapenda kuoneshauwepo wake wa karibu kwa wale wote walioguswa na mkasa huu.

Baba Mtakatifu katika ujumbe ulioandikwa kwa niaba yake na Kardinali Pietro Parolin, Katibu mkuu wa Vatican kwenda kwa Rais Recep Tayyip Erdogan wa Uturuki anasema, anapenda kuziombea roho za marehemu na kuwatia shime wale wote wanaoomboleza kwa kuondokewa na ndugu, jamaa na marafiki zao. Baba Mtakatifu anawavipongeza vyombo vya ulinzi na usalama kwa huduma ya upendo waliyoionesha kwa watu walioguswa na maafa haya mazito. Baba Mtakatifu Francisko mwishoni, anawaombea neema na baraka, amani na uponyaji, ili Uturuki iweze kuimarika zaidi!

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S.

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican.








All the contents on this site are copyrighted ©.