2016-03-10 08:28:00

Mhubiri ; 'kugawana ni kuzidisha


Katika Mahubiri ya sita  kwa ajili ya mazoezi ya kiroho ya kipindi cha  kwaresima kwa Papa Francisko  na wasaidizi wake, mada ya uwazi katika  mali  na haja  ya kugawana na wengine tulivyo navyo, ilikuwa ni vipengere  muhimu, vilivyolengwa na Mhubiri Padre Ermes RonchI, katika mafungo ya Kiroho kwa Papa na wasaidizi wake. . Mazoezi yaliyoanza Jumatatu  katika kituo cha kiroho cha Araccia nje kidogo ya jiji la Roma. Sehemu kubwa ya tafakari za Mhubiri, inatazama  maswali yaliyoulizwa na Yesu kama ilivyoandikwa katika vitabu vya Injili.  

Kwa Jumatano asubuhi Mhubiri alitafakari swali la Yesu : mna mikate mingapi? (Marko 6:38, Mathayo 15:34).  Padre Ronchi alilenga zaidi katika suala linalochukiza Wakristo wengi , kuona viongozi wa Kanisa kushikamana na fedha , badala ya kufurahia kugawana mkate walio nao na wengine. 

Padre Ronchi alitazama kwa makini, njaa ya kubwa  ya watu wengi , si kwa chakula tu cha kimwili lakini hata njaa ya kiroho pia  ,  wengi ambao  Mungu  hawezi onekana isipokuwa katika umbo la chakula. Aliendelea kueleza hisia hii ya njaa inavyoweza kuufisha mwili kama haikuzimwa kwa chakula  kama ilivyo kwa mwili na kiroho pia. Na kwamba Maisha , huanza kwa kusikia njaa , kuishi ni kusikia njaa, alieleza na kuwatazamisha waliokuwa wakimsikiliza  katika mazingira ya mamilioni ya watu duniani wanaokabiliwa na njaa na umaskini, mamilioni ya mikono inayoonyosha kuomba kitu cha kula, akisema hii haihitaji ufafanuzi wa kidini  ni swala lililowazi na kanisa linapaswa kutoa jibu lake.

Akinukuu kutoka somo la Injili linalozungumizia kuzidishwa kwa mikate na samaki , Padre Ronchi anasema Yesu anatutaka kuwa wakweli  kaiak mali tulizo nazo. Yesu anawauliza wanafinzi wake mna mikate mingapi?  Anataka kusikia  ukweli kwa kuwauliza wanafunzi wake kile walicho nacho mkononi. Na ndivyo ilivyo hata leo kwetu kama  wafuasi wa Yesu, tunaulizwa  idadi ya mali walizonazo.  Kiasi gani cha fedha ? Nyumba ngapi, magari mangapi, vito tulivyo navyo ,  na hata kiwango cha maisha tunayoishi ? Haya yote ni lazima kuyafanyia tathimini kwa kujilinganisha na watu wa kawaida wanaowanyoshea mikono yao walau hata kidogo tu za kulinda uhai wao.

Padre Ronchi alikamilisha mahubiri yake akisema hakuna sababu za kuogopa au kuhofu kutaja  wazi  mali tulizo nazo , maana Yesu anatutaka kufanya hivyo.  Yesu  anauliza unamikate migapi?  Kuwa wazi maana yake ni kuwa mkweli . Na  ukweli humweka mtu kuwa huru.  Ni huru kwa sababu hana alichoficha yote,  ni wazi na yu tayari kugawana na wengine kama anatakiwa kufanya hivyo.

Katika hili, ameifafanua mantiki ya Yesu kwamba ni kutoa na si kuhodhi.  Na kwamba upendo wa Injili maana ya ni kutoa  kama inavyoonekana katika muujiza huu wa kuzidisha mikate na samaki . Huu ni utendaji wa siri ya Mungu inayoufanya  mkate mmoja kuwa ni mkate wa wote . Unakuwa ni chakula cha kinachokidhi njaa  na kusaza.  Kwa muujiza huu wa mkate na samaki,  tunapata fundisho kwamba njaa ya wengine ni njaa yetu pia. 








All the contents on this site are copyrighted ©.