Kwa muda wa siku tano tangu Machi 07-11 mjini Dakar Senegal kunafanyika mkutano wa mwaka wa Bodi ya Wakurugenzi wa Taasisi ya Yohana Paulo II kwa ajili ya nchi za Ukanda wa Sahel ( Burkina Faso, Cape Verde, Niger, Chad, Senegal, Mali, Guinea Bissau, Mauritania na Gambia ). Bodi iliyoanzishwa tangu mwaka 1984 na Mtakatifu Yohane Paulo II, kama mkono wa Baraza la Kipapa linaloratibu misaada ya Kanisa Katoliki kwa ajili katika kukidhi mahitaji yalazima kwa watu wahitaji wa Ukanda wa Sahel
Baadhi ya Wajumbe wa Bodi hii ni Askofu Sanou Lucas Kalfa, wa Banfora (Burkina Faso), Mwenyekiti wa Bodi; Askofu Paul Abel Mamba, wa Ziguinchor (Senegal), Makamu Mwenyekiti;Askofu Martin Albert Happe, wa Nouakchott (Mauritania), mweka hazina; Askofu Ambroise Ouedraogo, wa Maradi (Niger).; Muadhama Kardinali Arlindo Gomes Furtado, Askofu Mkuu wa Santiago ya Cape Verde (Cape Verde), Askofu Djitangar Edmond, wa Sarh (Chad); Askofu Elison Robert Patrick wa Banjul (Gambia); Askofu Pedro Carlos Zilli, wa Bafata (Guinea Bissau); Askofu Augustin Traore, wa Segou (Mali).
Katika mkutano huu, pia anashiriki Katibu mkuu wa Cor Unum, Padre Giampietro Dal Toso, kama Mtazamaji wa Jimbo la Takatifu. Mkutano kati ya mengine pia unafanya mapitio katika miradi iliyopendekezwa inayosubiri kupata fedha . Kwa mwaka 2015 jumla ya miradi 91 miradi ilipata ufadhili kwa gharama ya karibu $ milioni 1.
Taasisi hii hufanikishwa kwa ushirikianao na Baraza la Maaskofu la Italia, Baraza la Maaskofu la Ujerumani, na makanisa na jumuiya za kijamii, ambazo hutoa msaada kwa niaba ya Baba Mtakatifu kwa ajili ya jamii inayoishi katika mkoa huo wa sahel . Lengo la juhudi hizi hasa ni kupambana na kuenea kwa jangwa. N a hivyo miradi mingi inahusiana na sekta ya mazingira, usimamizi na maendeleo ya kitengo cha kilimo, mifumo ya kusukuma maji, uboreshaji wa maji ya kunywa, na nishati mbadala. Pia ina lengo la kutoa mafunzo ya ufundi , ili waweze kujitosheleza wenyewe kihuduma. Aidha taasisi hii imekuwa ni chombo muhimu katika ufanikishaji wa mazungumzano baina ya dini walengwa hasa wakiwa waumini wa dini ya Kiislamu.
Ripoti ya Maendeleo ya Binadamu kwa 2015, ambayo kila mwaka hutoa orodha ya maendeleo ya binadamu kwa kila nchi kutoka jumuiya ya kimataifa, ilionyesha kuwa miongoni mwa nchi 20 zilizo chini katika orodha hiyo, 17 za Kusini mwa dunia, saba za mwisho 7 ni kutoka eneo mkoa wa Sahel, ambazo ni miongoni mwa mikoa maskini duniani. Inakadiriwa, Sahel yenye kuwa na jumla ya watu milioni 100,kati yao milioni 24 huishi katika hali umaskini uliokithiri na hasa lishe duni inayosababisha watoto milioni 6 wenye umri chini ya miaka 5 kukabiliwa na utapiamlo. Moja ya matatizo makuu yanayosababisha hali hiyo ni kupungua kwa maliasili: kwa mfano, Ziwa Chad, ambalo huunganisha mipaka Nigeria, Cameroon, Niger na Chad likiwa pia na aridhi inayowalisha watu zaidi ya milioni 2.5, limepungua kwa karibia asilimia 80% ikilinganishw ana lilivyokuw aktika miaka ya hamsini. Aidha eneo hilo limekuwa na matatizo makubwa ya makundo ya ugaidi na utekaji nyara, na hivyo kulifanya eneo hilo kuwa mahali pa hatari kwa maisha ya kawaida
Hadi mwaka 2014, jumla ya miradi 3100 ilifadhiliwa na Mfuko wa Yohane Paul II ukitumia zaidi ya $ 36 milioni zilizotengwa, kwa ajili ya Ukanda wa Sahel.
All the contents on this site are copyrighted ©. |