2016-02-27 12:15:00

Sheria ni msumeno!


Waziri Mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa amesema agizo lilitolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli la kuwataka mawaziri ambao hawajajaza Tamko la Rasilimali na Madeni wakamilishe kabla ya saa 12 Ijumaa limetekelezwa. Katika sakata hili la kimaadili, mawaziri watano wameponea chupuchupu kupambana na mkondo wa sheria.

Waziri Mkuu amepokea barua kutoka kwa Kamishna wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Jaji (Mst.) Salome Kaganda ikithibitisha kuwa mawaziri na naibu mawaziri wote wametekeleza agizo hilo. “Hadi kufikia saa 9.30 leo alasiri (Ijumaa, Februari 26, 2016) mawaziri wote walikuwa wamekamilisha fomu zao za kuzikabidhi katika Ofisi za Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma,” alisema Waziri Mkuu.

Rais Magufuli leo asubuhi alitoa maelekezo kwamba Mawaziri ambao hawajajaza Tamko la Rasilimali na Madeni ifikapo leo Ijumaa tarehe 26 Februari, 2016 saa 12.00 jioni wawe wamejaza na kurejesha Fomu ya Tamko la Rasilimali na Madeni katika Ofisi za Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Dar es Salaam. Waziri ambaye atashindwa kutekeleza agizo hili atakuwa amejiondoa mwenyewe kwenye nafasi yake.

IMETOLEWA NA:

OFISI YA WAZIRI MKUU.








All the contents on this site are copyrighted ©.