2016-02-23 08:09:00

Rais Museveni wa Uganda kaibuka kidedea!


Tume ya uchaguzi nchini Uganda imemtangaza Rais Yoweri Kaguta Museveni kuwa ni Rais wa Uganda baada ya kushinda kwenye uchaguzi mkuu uliofanyika hapo tarehe 18 Februari 2016 kwa kujipatia asilimia 60% ya kura zote halali zilizopogwa. Mpinzani wake wa karibu aliyemtoa jasho Museveni wakati wa kampeni n Dr. Kizza Besigye amejipatia asilia 35% ya kura zote.

Hata hivyo, Jukwaa la upinzani nchini Uganda linapinga matokeo haya kwa kusema kwamba, haki haikutendeka kwani Dr. Besigye kwa muda wa siku mbili alikuwa amezuiliwa nyumbani kwake. Uchaguzi mkuu nchini Uganda umefanyika katika mazingira tete kutokana na uwepo wa matukio ya uvunjaji wa sheria, ucheleweshaji wa vifaa vya kupigia kura pamoja na Serikali kuzuia matumizi ya mitandao kwa wananchi wa Uganda.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S.

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican.








All the contents on this site are copyrighted ©.