Jumapili ya Pili ya kipindi cha kwaresima, kabla ya sala ya Malaika wa Bwana, Baba Mtakatifu Francisko , katika tafakari yake fupi kwa mahujaji na wageni, waliokusanyika katika Uwanja wa Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro Vatican, alitafakari ziara yake ya kitume nchini Mexico.
Papa alianisha uzoefu alioupata katika ziara hiyo na yaliyoandikwa katika somo la Injili juu ya tukio la Yesu kubadilika sura akisema kuwa , pia wakati wa ziara yake ya Mexico , aliweza ona mabadiliko, kwa Bwana kumwonyesha mwanga wa utukufu wake, kwa njia ya mwili wa Kanisa lake, la Watu Watakatifu wanaoishi katika nchi ya Mexico.
Alirudia kutaja nia ya hija yake Mexico kwamba, ilikuw ani kwenda kuhiji katika Madhabahu ya Mama yetu wa Guadalupe. Kutafakari mbele ya sanamu hiyo ya miujiza, upendo na huruma ya Bikira, ambaye mahujaji wengi hufika mbele yake, wakiwa wamejawa na yote mioyoni mwao , furaha , huzuni na mateso mengi, kutoka bara lote la Amerika, kwa nia ya kuomba msaada, tokea mahali hapo ambapo Bikira huyo wa Morenita mwenyewe, alijionyesha kwa Juan Diego Mhindi mwekundu, kama mwanzo wa uinjilishaji kwa bara la Amerika ya Kusini na mwanzo wa ustaarabu mpya kama matunda ya kukutana kwa tamaduni mbalimbali. "
Papa alitaja hilo kuwa ndiyo urithi wa kweli Mexico walioupokea kutoka Bwana, kudumisha utajiri wa utofauti, na, wakati huo huo, kudhihirisha umoja katika imani moja. Papa Francis akiw aMexico alisema yuko Mexico, kama ilivyokuwa kwa watangauzlizi wake , kuimarisha imani ya watu Mexico, lakini pia nao kuthibitisha imani yao. Maelezo ya Papa yalilenga katiak ushuhuda uliotolewa na watu wa Mexico ikiwa ni familia, vijana, Mapadre na Watawa, Wafanyakazi na Wafungwa kwamba, ulikuwa ni ushuhuda wa imani ya wazi na imara, ushuhuda wa imani wanayoiishi, imani iliyobadilisha maisha yao .
Baada ya malezo hayo , Papa alitoa shukurani zake za dhati kwa Bwana na kwa Bikira wa Guadalupe, kw akumjalia safari nema na pia alitoa shukurani zake kwa wale wote waliohusika katika kazi za maandalizi na mipango yote iliyofanikisha ziara yake Mexico, ambayo ameitaja kwamba imekuwa ya mafanikio.
Na mwisho alitoa shukurani kwa Utatu Mtakatifu , uliomwezesha kukutana na ndugu yake mpendwa katika Kristo, Patriaki Kirill, Askofu Mkuu wa Kiekumeni wa Moscow na Urusi yote , mkutano uliofanyika Havana Cuba wakati akielekea Mexico. Na alihitimisha na ombi kwa Mama wa Mungu , aendelee kuwaongoza katika njia ya kutembea pamoja kwa umoja kamili kama wafuasi wa Mwana wake Yesu Kristo
All the contents on this site are copyrighted ©. |