2016-02-17 14:58:00

Askofu mkuu Robert Ndlovu ateuliwa kuwa msimamizi wa Kitume Chinhoyi


Baba Mtakatifu Francisko amekubali ombi la kung’atuka kutoka madarakani lililowasilishwa kwake na Askofu Dieter Bernd Scholz wa Jimbo Katoliki Chinhoyi, Zimbabwe kadiri ya Sheria za Kanisa namba 401 § Ibara ya 1. Wakati huo huo, Baba Mtakatifu amemteua Askofu Mkuu Robert Christopher Ndlovu wa Jimbo kuu la Harare, Zimbabwe kuwa Msimamizi wa Kitume wa Jimbo Katoliki la Chinhoyi, Zimbabwe.








All the contents on this site are copyrighted ©.