Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bwana Ban Ki moon , Ijumaa iliyopita katika mkutano wa wahisani wa kimataifa, uliofanyika mjini Addis Ababa , aliihimiza Jumuiya ya kimataifa, kuunganisha nguvu na mataifa yanayokabiliwa vibaya na ukame , kwa mfano Ethiopia, hasa katika kukabiliana na majanga asilia kama ukame wa kukithiri, unaosababisha maelfu ya watu kukosa chakula . Bwana Ban alikuwa mjini Addis Ababa kwa ajili ya kushiriki katika Mkutano wa 26 wa Umoja wa Afrika. Ban Ki moon pia alitembelea maeneo yaliyokumbwa vibaya na ukame Ethiopia, ukame unaotajwa kuwa matokeo ya El Niño na athari za mabadiliko ya tabianchi.
Katika mkutano na wahisani , Ban alikiri uwepo wa dharura nyingi zinazokabili Serikali za nchi zinazokumbwa na majanga asilia kama El Niño, akionyesha kujali kwamba, kwa bahati mbaya hali hizo hazitabiliki asilimia kwa mia.
Alieleza na kupongeza uongozi wa serikali ya Ethiopia, kwa jinsi ulivyoweka mkazo katika kukabiliana na matokeo ya janga hilo la ukame mpaka sasa. Na akataja nia za Umoja wa Mataifa, kwa kushirikiana na Benki ya Dunia, kuunga mkono Mpango wa serikali, unao wania kutoa msaada kwa watu milioni nane, walio katika hatari kubwa za kukabiliwa na ukosefu wa chakula na fedha, kutokana na hali ya ukame . .
Aidha KatibuMkuu alisifu juhudi za kimaendeleo zinazofanywa Ethiopia katika miaka ya hivi karibuni kwamba zinavutia kusaidia taifa hilo, hasa katika uimarishaji na usambazaji wa mitandao ya miundombinu kwa jamii na kwa ajili ya ujenzi wa ujasiri wa kitaifa kwa siku zijazo, kama ilivyokubalika katika Malengo ya Maendeleo Endelevu , hakuna wa kubakishwa nyuma, iwe katika Pembe ya Afrika au kwingineko. Katibu Mkuu Ban Ki moon, alieleza akisiema , uwepo wa migogoro na vipeo ni vikwazo vikubwa katika ufanikisha wa Ustawi na maendeleo ya kudumu kwa wote.
Katibu Mkuu aliweka matumiani yake katika Mkutano wa Dunia juu ya ubinadamu, utakaofanyika mjini Istanbul tarehe 23 na 24 Mei 2016, kama ni fursa kwa waliopiga hatua za kwanza katika maendeleo kusaidia waliobakinyuma.
All the contents on this site are copyrighted ©. |