Ijumaa hii katika kukamilisha mkutano wake, wajumbe wa Baraza la Kipapa la Mafundisho tanzu ya Kanisa walikutana na Baba Mtakatifu Francisko katika ukumbi wa Clementina hapa Vatican. Papa katika hotuba yake, alilenga zaidi katika mambo matatu; mwingiliano wa uhusiano wa kazi za matendo ya huruma kiroho na kimwili; umuhimu wa utendaji wa pamoja katika maisha ya kazi na uongozi , na tunu za hirakia ya uongozi katika maisha na utume wa kanisa.
Pamoja na kutoa shukurani zake za dhati kwa watendaji wote wa kazi za shirika hilo na washauri wake, pia Papa ameonyesha matumaini yake kwamba, katika kipindihiki cha Jubilee ya Mwaka Mtakatifu, waamini wote wa Kanisa wataweza kuhuisha upya imani yao kwa Yesu Kristo, ambaye ndiyo sura ya huruma ya Baba, na njia inayo unganisha Mungu na mwanadamu. Hivyo huruma inakuwa ni msingi wa maisha ya Kanisa yaliyosimikwa katika ukweli wa kwanza wa Kanisa, ambao ni upendo wa Kristo.
Kwa mtazamo huo, Papa alihoji kwa vipi inaweza kukosekama kwa Wakristo, wachungaji na walei, hamu ya kutaka kugundua na kuweka matendo ya huruma kama kiini cha utendaji wote katika kipindi hiki cha Jubilee, katika maisha ya kawaida na kiroho pia. Papa ameeleza na kuonya kwamba, mwisho wa safari hii ya maisha, tutapaswa kujibu, iwapo tuliweza kulisha na kunywesha wenye njaa na kiu, sawia kutakuwa na swali jingine iwapo tuliweza kuwasaidia watu kutoka katika hali zao za mashaka na na kuwapokea wenye dhambi , kuwaonya au kurekebisha mienendo yao, na hasa sana katika masuala yanayohusiana na habari za imani ya Kikristo na maisha mazuri.
Hotuba ya Papa iliendelea kurejea kazi msingi iliyokabidhiwa shirika, kueleza kwa ufanisi upendo na huruma, ambavyo huuunganisha Mungu na binadamu, kupitia Yesu Kristo, ambaye ni utimilifu wa huruma na upendo wa Mungu, uliotolewa kwa ajili ya wokovu wa watu. Papa ametaja hiyo ndiyo kazi kuu ya Shirika walilokabidhiwa, na hapo ndipo kuna msingi wake na ukweli wote. Imani ya Kikristo, kwa kweli, si tu maarifa yaliyohifadhiwa katika nyaraka na vitabu vya kumbukumbu, lakini ni ukweli wa kuishi katika upendo. Kwa hiyo, pamoja na mafundisho ya imani, mtu lazima kulinda uadilifu wa maadili, hasa katika mazingira nyeti ya maisha. Mshikamano wa imani katika nafsi ya utu wa Kristo, ina maana ya kutoa majibu yote kwa kuzingatia tunu zote za kimaadili. Kwa mtazamo huo, Papa alitoa shukurani zake kwa wote waliohusika na utoaji wa majibu yanayofaa katika juhudi za kukabiliana na kesi watoto kutumiwa vibaya na viongozi wabovu wa kanisa.
Papa alieleza na kurudia kuzungumzia umuhimu wa Huduma za kanisa kufanyika kwa uadilifu wa imani na maadili kwamba ni muhimu katiak mazingira yote ya kiimani na kanisani . Na kwa kutimiza utume huu, ni muhimu kutenda kazi zote kwa pamoja. Adiha Papa ametoa shukurani na pongezi zake kwa wale wote wanaotoa mchango wao muhimu kwa Shirika , kwa kazi yao nzuri na unyenyekevu , na hivyo amehimiza waendelee na moyo huo kama ilivyokuwa katika kushughulikia mada za mkutano wa Shirika uliokamilika.. Papa amesema, kuna haja ya kukuza, katika ngazi zote za maisha ya kanisa, umoja na haki.
Papa ameshauri uwepo wa mikutano kama uliofanyika mwaka jana, uliokutanisha wajumbe kutoka Mabaraza Katoliki ya Maasskofu ya Ulaya, kujadili kw apamoja jinsi ya kukabiliana na baadhi ya changamoto dhidi ya Mafundisho na kazi za Kichungaji za Kanisa. Papa anasema , njia hii inaweza saidia kuinua ari mpya kwa waamiini na umisionari mpya , hasa katiak mataifa ya Ulaya ambako roho ya ubinadamu inamomonyoka. Papa ameendelea kulitaka shirika kuendelea kuimarisha ushirikiano na tume za ushauri kutoka Mabaraza ya Maaskofu, na pia Maaskofu kama mtu binafsi, pale panapo jitokeza wasiwasi kwa mafundisho ya kweli kutaka kuzonga na malimwengu , na wakati wa madai ya mabadiliko ya haraka, yenye kuongezeka utata katika wa hoja za kiimani.
Papa pia amezungumzia mchango wao muhimu katika kufanya upya maisha ya kanisa kupitia utafiti unaotafuta mkamilishano kati ya tunu za hirakia za utawala na karama. Papa amesema kwa mujibu wa mantiki ya umoja katika tofauti halali - mantiki yenye kuonyesha sifa ya kweli katika kila aina ya usharika halisi wa Watu wa Mungu, tunu za uongozi na karama , vimeitwa kufanya kazi pamoja kwa manufaa ya Kanisa na ulimwengu. Ushahuda huu wa kusaidiana, leo hii inakuwa ni hoja ya haraka zaidi kuliko ilivyokuwa kipindi cha nyuma, ikidai kila jumuiya a kanisa, kuonyesha sifa zake kama kielelezo cha jamii iliyoridhiana, yenye kuishi katika Kiini cha umoja wa Utatu wa Mungu na kama zawadi kutoka kwa Baba, Mwana Roho Mtakatifu. Papa anasema Umoja na wingi ni uthibitisho wa Kanisa ambalo,huongozwa na Roho Mtakatifu, lenye kutembea kwa aminifu katika hatua zake zote, kuyaelekea malengo yaliyowekwa na Bwana Mfufuka , yenye kuonyesha mwendo na historia ya kanisa. Papa ameeleza na kutoa mfano wa mikutano ya sinodi ,kama tunda la umoja na ushirikiano wenye kuongoza katika umoja halisi wa kina na mpana zaidi katika huduma ya maisha na utume wa watu wa Mungu .
All the contents on this site are copyrighted ©. |