2016-01-27 14:43:00

Papa - Mungu husikia kilio cha watu wake


Katekesi ya  Baba Mtakatifu Francisko,  kwa mahuaji na wageni, imeendelea kuvuviwa na uwepo wa maadhimisho ya Mwaka Mtakatifu wa Jubilei ya huruma ya Mungu. Jumatano hii,  ametafakari  uwepo wa  huruma ya Mungu katika  historia ya watu wateule, akitazama kwa makini jinsi huruma ya Mungu alivyowakomboa wana wa Israel kutoka utumwani Misri. .  

Akihutubia katika lugha ya kiitaliano , alisema kuwa kwa huruma yake, Bwana anaandamana na watu wake katika katika njia yao ya maisha , akiwaongoza katika njia ya neema na maridhiano, kama yanenavyo Maandiko juu ya Yusufu na ndugu zake (Mwa 37-50).  Kwa aya hizo, Papa  alieleza jinsi ambavyo mawazo yake huwaelekea watu wengi waliolazimika kuwa mbali na familia zao au wale ambao mazungumzani tena.  Kwao wote ametoa ombi kwamba, katika  mwaka huu wa Huruma ya Mungu, waone kama  ni  fursa nzuri ya kukutana, kumkumbatiana  na kusameheana. Na uwe wakati wa kusahau  mabaya tuliyotendewa, kusamehe makosa yote ya nyuma .  Papa ameomba na kutoa wito kwa watu wote kutoifanya migumu mioyo kama ilivyokuwa kwa wana wa  Waisraeli, wakati Bwana anawakomboa kutoka utumwani Misri.  

Papa ametaja,  jinsi Maandiko  Matakatifu yanavyoonyesha Huruma ya Bwana, kwa taifa la Israel katika historia yake yote, tangu mwanzo wa kuitwa kwa  Abraham, aksiema huruma ya Mungu, kwa namna ya kipekee , inaonekana katika maisha ya kila siku ya Waisrael tangu wakitoka  Misri. Mungu alikisikia kilio cha watu wake, kama anavyokisia kilio cha  maskini na wanaogandamizwa  katika kila lika ktiak wakati wetu.  

Papa ameendelea kueleza jisi alivyo mteua  Musa  kuwa mjumbe wake wa huruma na wokovu. Jinsi kupitia kwa  Musa, alivyo waongoza Wana wa Israel katika  uhuru na kwa njia ya ahadi yake, aliwafanya kuwa taifa lake mwenyewe teule. Ufalme wa  makuhani na taifa takatifu" (Kut 19: 5-6),watu wenye  thamani machoni pake.

Papa aliendelea kutafakari juu ya fumbo la huruma ya Mungu, akisema, lilifikia upeo wake kamilifu kwa kumutuma Mwana wake pekee, Yesu Kristo kkwa agano jipya na la milele, kwa kumwanga damu yake msalabani , , ambamo tunapata msamaha wa dhambi zetu na kuwa kweli ,watoto wa Mungu, wana wapendwa wake, Baba Yetu mwema na Mwenye Huruma wa mbinguni.

Na hvyo nasi pia katika mwaka huu wa Huruma ya Mungu, tunaweza kufanya kazi hii kuwa wapatanishi wa huruma kwa matendo ya huruma yenye kutuweka karibu na kuwa wafariji na wajenzi wa umoja . Papa anasema kuna mambo mengi mema tunayoweza fanya, katika kuionyesha huruma ya Mungu, ambayo daima ni kwa ajili ya kuokoa, ikiwa kinyume kabisa na wale wanaopenda kuua au kufanya uhalifu mfano wale wanaopendelea vita.

Papa amesisitiza, iwapo sisi ni watoto wa Mungu,  basi tunayo haki ya kuwa warithi wa huruma hii . Na hvyo amemwomba  Bwana , neema za mwaka huu Mtakatifu, zituwezeshe sote kutenda mema, kuwa na matendo ya huruma, jna kufungua  mioyo yetu kwa ukarimu wa kumfikia kila mtu kupitia huruma ya Mungu pamoja nasi kama warithi wake.  








All the contents on this site are copyrighted ©.