2016-01-26 09:27:00

Madhabahu ya Mama Yetu wa Rozari ya Fatima, kufunguliwa upya


Gombera wa Madhabahu ya Mama yetu wa Rozari ya Fatima Ureno, ametangaza habari njema ya kukamilika kwa kazi za ukarabati na marekebisho, zilizokuwa zikifanyika katika Madhabahu ya Mama Yetu wa a Rozari ya Fatima Ureno,  kwamba  Madhabahu hayo, yatafunguliwa upya rasmi hapo tarehe  Februari 2, wakati wa adhimisho la Siku kuu ya Bwana kutolewa Hekaluni, sanjari na Siku ya Watawa Duniani.

Padre  Carlos Cabecinhas , ameviambia vyombo vya habari kwamba, ukarabati uliofanyika ni kwa  manufaa ya waamini wanatakao penda kutoa  heshima zao na kusali katika  makaburi ya Wenye Heri Francisco na Jacinta Marto yaliyoko  karibu madhabahu  kuu . Kwamba , kwa sasa  njia inayokwenda kwenye makaburi ya wachungaji wadogo waliotokewa na Mama Maria, ambayo awali  ilikuwa ikichanganya mahujaji, kwa  sada   imewekwa wazi zaidi na hivyo ni rahisi kufika katika makaburi hayo.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Katoliki SIR, Askofu wa Leiria-Fatima,  António Marto, ataongoza Ibada ya Misa  kwa nia ya kutabaruki   madhabahu mapya ,  hapo tarfehe 2 Februari 16, ya Kanisa Kuu la Mama Yetu wa Rozari wa Fatima.  Padre Cabecinhas ameendelea kueleza kwamba, baada ya  kufunguliwa kwa Basilika la Mama Yetu wa Fatima, Ibada za Misa zitakuwa zikisomwa kila siku kwa mahujaji . 

Kazi ya Michoro ya sasa katika Madhab ahu imefanywa na  msanii maarufu  Bruno Marques  kwenye Basilka hilo ambalo ujenzi wake ni ulianza mwaka 1928, kwa michoro ya  mtalaam wa majengo  wa Uholanzi,  Gerard Van Kriechen na kujengwa na  mhandisi wa Ureno  João Antunes.  Jengo hilo lililowekwa Wakfu  Oktoba 7, 1953, lina  urefu wa mita 70.5 na mapana ya mita 37, na liliwekwa  wakfu kwa Mama yetu wa Rozari na Papa Pius XII,  kwa hati yake ya Kipapa ya  "Luce Superna"  ya Novemba 11, 1954.








All the contents on this site are copyrighted ©.