2016-01-23 14:59:00

Balozi Matthew S. M. Lee awasilisha hati zake za utambulisho kwa Papa


Baba Mtakatifu Francisko, Jumamosi tarehe 23 Januari 2016 amepokea hati za utambulisho kutoka kwa Bwana Matthew S. M. Lee, Balozi mpya wa Taiwan mjini Vatican. Balozi Lee alizaliwa tarehe 1 Februari 1955 huko Penghu, Taiwan. Katika maisha yake amewaji luwa ni mtafsiri na mhariri wa Gazeti la China Times. Mfanyakazi katika Idara ya Itifaki na masuala ya mambo ya nchi za nje nchini Marekani. Katibu mkuu wa Ubalozi wa Taiwan nchini Marekani.

Kuanzia mwaka 1991 hadi mwaka 1994 alikuwa ni kiongozi mkuu wa Seneti C. J. Chen; Kaimu Balozi na Mshauri, Mkurugenzi wa habari na Mkurugenzi wa Mambo ya nchi za nje na ushirikiano wa kimataifa. Mkurugenzi na Mshauri mkuu huko San Francisko. Kunako mwaka 2005 hadi mwaka 2006 aliteuliwa kuwa Balozi wa Taiwan huko Lithuania: Mwaka 2006 hadi mwaka 2008, akateuliwa kuwa Balozi Jamhuri ya Palau.

Kuanzia mwaka 2009 hadi mwaka 2011 aliteuliwa kuwa Mkurugenzi mkuu wa mambo ya nchi za nje na ushirikiano wa kimataifa Asia Mashariki na Visiwa vya Pasific. Na Mwaka 2011 hadi mwaka 2014 alikuwa ni Balozi wa Taiwan nchini Argentina na mwishoni, kuanzia mwaka 2014 hadi mwaka 2015 alikuwa ni Balozi wa Taiwan nchini Yordan.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S.

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican.








All the contents on this site are copyrighted ©.