2016-01-15 14:26:00

Papa- kila Mbatizwa atathimini kiwango cha Imani yake kwa Kristo


 Baba Mtakatifu Francisko ametoa wito kwa Wakristo kutathimini imani yao kwa Kristo,  huku akisisitiza kuwa, ili kumwelewa Yesu , muumini anapaswa kuifunua roho yake wazi kwa Kristo , na kuruhusu kutembea pamoja na Kristo, katika njia ya msamaha na unyenyekevu wa moyo.  Papa alitoa himizo hilo mapema asubuhi wakati akiongoza Ibada ya Misa katika Kanisa dogo la Mtakatifu Marta hapa Vatican.  Papa aliitumia nafasi hiyo kuonya kwamba,   imani  hainunuliwi , bali  mtu huipata kama "zawadi" kwa  kufanya mabadiliko mazuri katika maisha.

Na kwamba watu wanaopenda kuwa karibu na Krato hufanya kila linalowezekana bila kufikiri hatari zinazowakabili kwa kufanya hivyo bali huiskiliza sauti ya ndani inavyodai .  Mafundisho ya Papa yalilenga katiak somo la Injili ya Marko, lililoeleza uponyaji wa yule mwenye kupooza kule Kafarnaumu. Papa amesema - imani sawa na ile mwanamke ambaye pia, katika umati wa watu, wakati Yesu alikwenda nyumbani kwa Yairo, alifanya kila jitihada hadi kugusa pindo la vazi la Yesu,  akiwa nai mani kwamba atapona.  Na ni Imani hiyohiyo alikuwa nayo akida aliyeomba mtumishi  uponywaji wa mtumishi wake. Hivyo Papa anasema Imani ni nguvu ya ajabu, ni  ujasiri wa kusonga mbele katika maisha kwa Mioyo ya iliyo wazi katika  imani.

Papa alieleza na kuwataka waumini kuiomba imani hii kutoka kwa Yesu, kwa ajili ya kupata mabadiliko ya kweli katika maisha.  Papa alionyesha kutambua nguvu ya Mungu yenye kutoa uponyaji katika maradhi ya kiwmili , lakini  akasema ni muhimu kwanza kabisa kuomba kuokolewa na maradhi ya kiroho ambayo ni dhambi. Ni kumwomba Bwana atuokoe na dhambi na kutuongoza kwa Baba Mbinguni. aliendelea kueleza jinsi Kristo  alivyoitikia kwa utii matakwa ya Baba Mungu,  ya kutoa maisha yake kwa ajili ya wokovu wa binadamu. Papa anasema, hili ni jambo gumu kulielewa kama ilivyokuwa pia vigumu kwa waandishi walioishi na Yesu kuelewa hilo na ndivyo ilivyokuwa hata kwa wanafunzi wake.

"Imani katika Yesu Kristo aliendelea , ni kusadiki kwamba Kristo anaweza kubadili mwenendo wa maisha . Ni kuamini kwamba Yesu Kristo ni Mungu, Mwana wa Mungu, aliyeyatolea maisha yake kwa ajili ya wokovu wa binadamu.  Na hivyo katika Mwaka huu maalum kwa ajili ya kuomba huruma ya Mungu, mwaka wa kuomba msamaha,na tuiombe zawadi hii ya imani, izidi  kushamiri katika roho zetu, ili tuweze kuwa na mabadiliko ya kweli  chanya  katika uliwmengu wa kiroho.  Ni lazima kutolea maombi yetu kwa uchaji na unyenyekevu na moyo wa  toba, kusema 'Nisamehe, Bwana. Wewe ni Mungu. Wewe waweze  kusamehe dhambi zangu.  Papa alieleza na kumwomba Bwana awajalie waamini wote kukua katika imani ya Yesu Kristo, kuwa ni nafsi ya Mungu, Msamehevu. Na atujalie mwaka wa neema, yenye kutuongoza katika kumtolea sifa na shukurani,Mungu ,  kwa wokovu wake. 








All the contents on this site are copyrighted ©.