Askofu Mkuu Janusz Urbanczyk , Mwakilishi wa Kudumu wa Jimbo la Papa katika Shirika kwa ajili ya Usalama na Ushirikiano wa bara la Ulaya (OSCE),na Mashirika mengine ya Kimataifa yaliyoko mjini Vienna, Alhamis 14 Januari 2016, alitoa mchango wa Jimbo la Papa katika Mkutano wa OSCE wa 1085,uliofanyika mjini Viena Austria.
Mwalikishi wa Jimbo la Papa, aliuambia Mkutano huo kwamba , mchango wa Jimbo la Papa, hauna majawabu ya moja kwa moja yanayweza kutoa ufumbuzi katika changamoto na hali ngumu zinazoonekana kuvuka mipaka ya uwezo wa dunia kwa wakati huu, lakini linahimiza na kuunga mkono nia zote zinazolenga kujenga uwanja wa majadiliano, mazungumzano na mipango mingine inayotafuta ufumbuzi uliobora zaidi, kuliko utumiaji wa mabavu, kudumisha amani na usalama duniani. Mwakilishi Vatican, alieleza kwa kutazama kwa makini hali ngumu zinazotikisa dunia kama mgogoro wa uhamiaji , akisema Jimbo Takatifu mpaka sasa linashukuru kwa juhudi kubwa za ushirikiano, unaoonyesha uwepo wa mshikamano na maskini wanaotafauta hifadhi na maisha yenye ubinadamu zaidi.
Aidha aliwarejesha washiriki wa mkutano huo, kutazama tatizo jingine linalokabili dunia leo, kuzorota kwa mazingira ya dunia. Askofu Mkuu Urbańczyk aliuambia mkutano kwa kutaja hamu ya Baba Mtakatifu Francisko katika kukabiliana na tatizo hili akiweka matumaini yake kwa Uenyekiti wa OSCE kwamba, utaweza pitisha hatua mpya makini na haraka kwa ajili ya matumizi endelevu ya rasilimali na kuwa na sauti thabiti katika usimamizi wa maliasili, ikiwa ni pamoja na kujaribu kila njia iwezekanavyo, kukomesha, haraka iwezekanavyo , kwa ubaguzi wa kijamii na kiuchumi katika mifumo yote ya kidunia.
Aidha Askofu Mkuu Urbańczyk, aligusia suala la jinsia, aksiema, Baba Mtakatifu Francisko, anasadiki, jinsia hizi mbili kiume na kike , tofauti zake , haziondoa usawa katika kuheshimu ubinadamu wa kila mmoja, kwa kuwa utofauti katika usawa, ni kirutubisho cha mmoja kwa mwingine, na ni muhimu kwa ajili ya umoja wa maisha katika jamii, na mwendelezo wa binadamu . Na kwamba Mwanamke ni ukamilifu wa Mwanamme na mwanamme ni ukamilifu wa mwanamke na uwepo wao hulega kukamilishana, si tu kimwili,na kisaikolojia, lakini pia katika mantiki za utu wa binadamu na maisha yake yote.
All the contents on this site are copyrighted ©. |