2016-01-14 14:20:00

Ujumbe wa Papa kwa Jubilei ya huruma ya Mungu kwa vijana wadogo


Mapema Alhamisi tarehe 14 Januari 2016, Vatican ilitoa ujumbe wa Baba Mtakatifu, wakati atakapokutana na vijana wadogo wenye umri kati ya miaka 13-16,wasichana na wavulana kwa ajili ya  Maadhimisho ya Mwaka Mtakatifu wa Jubilee ya Huruma ya Mungu. Adhimisho litakalofanyika rasmi Jumapili ya tarehe 24 Aprili 2016, ambayo itakuwa ni Jumapili ya IV katika kipindi cha Pasaka.

Ujumbe wa Papa kwa vijana hao wadogo, unawasisitiza vijana kuiona huruma ya Mungu kama  Baba . Na kwamba, maadhimisho  ya mwaka huu Mtakatifu wa Huruma ya Mungu, ni wakati wa kujichotea neema, amani, uongofu na maisha ya furaha. Ni wakati  unaotoa mwaliko kwa kila mmoja, kwa watu wa kila lika , wa mbali na karibu, kuiishi furaha hii, kwa kuwa hakuna kitu au sababu inayoweza kujenga ukuta au umbali, wa kuzuia huruma ya Baba Mungu kumfikia mtu yoyote na kumkumbatia.  Kwa ajili hiyo, Papa Francisko anasema MIlango Mitakatifu imefunguliwa katika majimbo yote ya Dunia , Roma na  kwingineko  ulimwenguni.

Ujumbe wa Papa anaendelea kuwahimiza vijana wanaopevuka kwamba, wakati wao pia unawataka washiriki katika  kikamilifu katika maadhimisho haya , wakiwa wamejawa na utambuzi kwamba,  kila mmoja wao ni mtoto wa Mungu.  Na kwamba anapenda kutoa huu kwa kumtaja kila kijana kwa jina lake , kuwaita kwa jina mmoja baada yamwingine  kama Yesu anavyofanya  kila siku.  Na kwamba anatambua kuwa majina yao yameandikwa mbinguni  na  katika moyo wa Baba,ambaye ndiye Roho ya huruma, na chanzo chote cha  maridhiano na wema.

Baba Mtakatifu ameendelea kuuzungumzia Mwaka huu mzima wa kuomba Huruma ya Mungu  kwamba kila wakati inakuwa ni nafasi kwetu kukua katika utakatifu. Ni  wakati ambamo tunaweza  kugundua kwamba,kuishi pamoja kama kaka  na dada, huleta furaha kubwa, ni  wakati wa tamasha zuri, na wakati wa sherehe isikuwa na mwisho, tuliyofundishwa  kusherehekea na Yesu katika Roho yake.  Kwa hiyo Jubilee ni  kushereheka  pamoja  na Yesu, ambaye anatoa mwaliko kwa kila mmoja wao, bila kumbagua yoyote. Na ndiyo maana Papa anaendelea kusema, katika ujumbe huu  anapenda kuwa na vijana hawa wadogo kwa siku kadhaa, kwa nao pamoja katika sala, ibada,  na matamasha ya pamoja.  Papa ameonyesha matumaini yake kwamba, vijana wengi wataungana naye hapo mwezi Aprili, kama anavyotamani iwe.  

Papa ameendelea kuwaasa vijana kwamba, Huruma ya Mungu ni sawa na Baba. kama inavyotaja Mada ya Jubilee hii. Na ni wakati wa kusali pamoja na kuwa karibu na Yesu.  Aidha amefafanua, nini mana ya kuwa mtu wa Huruma akisema, ina maana ya kukua katika upendo wenye ujasiri, ukarimu na halisi. Ina maana ya kukua kimwili na kiroho.  Ina maana kwao vijana kujiandaa vyema na kuwa imara katika  kutoa maamuzi ya  uchaguzi wao kama Wakristo , katika  ujenzi wa maisha ya kila siku, si kwa masuala makubwa tu lakini pia katika  mambo mengine madogomadogo, kwa ajili ya ufanikishaji dunia ya amani.

Ujumbe wa Papa aunendelea kuwaasa vijana kwamba, katiak nyakati hizi zao za maisha zimejaa mabadiliko mengi ya kushangaza. Ikionekana kama vile kila jambo linawezekana na wakati huohuo ikionekana kama hakuna linalowezekana kufanyika mara moja. Na hivyo, amerudia  kuwakumsha vijana kwamba ni muhimu wakabaki imara katiak nji ayao ya imani , kubaki na tumaini thabti kwa Bwana. Na hiyo ndiyo siri ya mafanikio katika safari yao ya maisha.Kwamba Bwana huwapatia ujasiri wa kusonga mbele kwa furaha dhidi ya mawimbi ya kidunia. Ni lazima wawe macho na mwelekeo wa mawimbi hayo. Ni lazima kutokubali kmepeprushwa nayo lakini kwenda kinyume na mwelekeo huo , kwa ajili ya manufaa ya kiroho . Na hakuna sababu za kuhofia kwa kuwa Yesu atawapa ujasiri huo. Wakiwa na Yesu wataweza kufanyamengi makubwa .Na ni yeye anayewapa furaha ktiak kuwa wafuasi wake ,na mashahidi wake. Papa amesisitiza na kuwataka wakabidhi nia zao kwa mambo yaliyo ya muhimu zaidi. Na kwamba, kama Wakristo hawakuchaguliwa na Bwana kwa ajili ya mambo madogomadogo , lakini kwa yaliyo makubwa . Na hivyo ni muhimu kuyaweka masiha yao kwa yaliyo ya muhimu.  

Katika ujumbe huo, Papa hakiìusahau kutaja wale ambao kwa wakati huu wanaishi katika mazingira magumu yanayosababishwa na uwepo wa  vita, umaskini uliokithiri, matatizo ya kila siku na upweke.  Katika hili Papa ameotoa wito kwa vijana kutopoteza matumaini!  Bali wadumu katika imani kwamba Bwana ana mpango nao., na yupo tayari kuwasidia .

Papa akionyesha kutambua kwamba sivijana wote wa umri wao, watakaoweza kufika Roma, na hivyo amewataka watakaoshindwa kuja Roma , kufanya maadhimisho haya katika makanisa hayo mahalia. Na wote wanaalikwa kukishiriki kipindi hicho cha furaha cha mwaka wa Jubilee ya Huruma kwa moyo wa kweli na kiakili pia.  Na wafikirie kwa makini juu ya matumaini na hamu yao watakayopenda kukabidhi kwa Kristo kupitia Sakramenti ya Upatanisho na Ekaristi watakapokuwa wakisherehekea kwa pamoja. Na kwamba, wakati wa kupita katika Mlango Mtakatifu, wakumbuke, hatua hiyo inawakumbusha umuhimu wa kukua katika  utakatifu na kujilisha kwa Injili na Ekaristi; Neno na Mkate wa maisha na kwa ajili ya kusaidia kujenga  dunia ya haki  na mshikamano  duniani.

Papa anaukamilisha ujumbe wake kwa kuomba Baraka za Bwana, ziwaongoza Vijana  kuelekea Mlango Mtakatifu, wao wenyewe na familia zao na katika kukua  katika wema na neema. Pia ameomba maombezi ya Bikira Maria , Mama wa watu wote, Mlango wa kweli wa Huruma.

 

 








All the contents on this site are copyrighted ©.